Wengi wa watu waliofariki ni wananchi wa Iran na Afghanistan
Vyombo
vya usalama vya Iraq vimesema kwamba zaidi ya watu themanini wameuawa
kwa shambulizi la bomu lililowalenga madhehebu ya kiislamu ya kishia
kusini mwa mji wa Baghdad.
Gari
lililokuwa limebeba vilipuzi hivyo lililipuka karibu na kituo cha mafuta
ambapo watu wengi wa dhehebu hilo walikuwa wameegesha magari yao.
Wengi wa watu waliofariki ni wananchi wa Iran na Afghanistan.
Walikuwa wakitoka kwenye moja ya tukio muhimu la kidini kwenye mji mtakatifu wa Karbala.
Mamia ya washiha hufanya hija katika mji wa Karbala
Askari wa kundi la kiislam wamekiri kuhusika na shambulizi hilo.
kundi hilo la wapiganaji la kiislam mara kwa mara hulenga madhehebu ya kishia na kuwatuhumu kwamba ni waongo.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment