Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Mt. Meru Millers mara baada ya kufanya ziara kiwandani hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa taarifa kwa Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan juu ya maendeleo ya kiwanda pamoja na changamoto wanazokutananazo wafanyabiashara wazawa.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka
kiwanda cha Mt. Meru Miller kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya
Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa ufafanuzi juu ya malighafi hizo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka
kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akingalia ndoo za plastiki zinazotengenezwa na kampuni ya Mt. Meru
Millers kwa ajili ya kuhifadhia mafuta ya kula ,kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
Serikali inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye
viwanda kama hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza
uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa watanzania.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha baada ya
kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru
Millers ili kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali
iweze kuzifanyia kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta
ya kupikia nchini.
Makamu wa
Rais amesema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda
hazina uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka
kuweka utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi
ambazo ni kero kwenye viwanda.
Amesisitiza
kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha viwanda vingi
vinajengwa nchini ambavyo vitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini
hali ambayo itasaidia uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi
kuuzwa kwenye masoko ya nje ya nchi na kuliingizia taifa mapato na
kuongeza ajira kwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ambazo anafanya kwenye viwanda
mkoani Arusha ni kujionea jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi za
uzalishaji na pale kwenye changamoto zinazokwamisha viwanda hivyo
kufanya kazi vizuri ziweze kufanyia kazi na Serikali.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul
Mittal amesema kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi
wanazotozwa kwenye Viwanda hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu
uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania.
Amesema
kwa sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa
Tanzania pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi
katika maeneo mbalimbali nchini.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment