Katibu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus
(kulia), akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya
Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Lengo
lilikuwa ni kuimarisha mabaraza hayo kwa ajili ya utendaji kazi wake
ikiwemo kuhakikisha wanachama wapya wanaendelea kujiunga na chama
chadema ili kukifanya kuendelea kuwa chama cha upinzani chenye nguvu
nchini.
Chama
hicho kililaani zoezi la kuwahamisha machinga kutoka katikati ya Jiji la
Mwanza huku mazingira rafiki yakiwa bado hayajaandaliwa ambapo Micus
alisema hatua hiyo inaweza kusababisha vijana na akina mama wengi kukosa
mwelekeo wa kujitafutia kipato kwa njia sahihi ambapo walihimiza
machinga hao kutengenezewa mazingira bora ya kufanyia biashara zao.
Na BMG Habari
Baadhi ya
viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack
Micus (kulia), wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza
ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Diwani wa
Kaya ya Butimba, John Pambalu, akizungumza juzi kwenye semina kwa
viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya
viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza diwani
wa Kata ya Butimba, John Pambalu, wakati akizungumza kwenye semina kwa
viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya
viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana, wakifuatilia kwa
makini semina iliyotolewa kwa ajili ya kuimarisha uhai katika utendaji
wao wa kazi ili kujiimarisha zaidi.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment