Mkurugenzi
wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye
makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akizungumza kwenye uzinduzi
wa Unga wa Viazi Lishe uliofanyika hii leo Jijini Mwanza. Taaisisi
hiyo imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia
vyombo vya habari.
Unga wa
viazi lishe ni muhimu kiafya kwani una wingi wa vitamini A miongoni mwa
vitamini mbalimbali ambapo husaidia kuondokana na matatizo ya kuona
(upofu). Pia viazi hivyo hutumika kama chakula, na unga wake ni bora kwa
ajili ya utengenezaji wa mandazi, chapati, keki, biskuti na vitafunwa
vya kila aina.
Taasisi
hiyo imeshirikia kama miongoni mwa taasisi hususani za wajasiriamali
wanawake zinazojihusisha na kilimo ikiwemo mbogamboga na matunda. Lengo
lake ni kuhakikisha wanawake wanajiinua kiuchumi ili kuondokana na
utegemezi na hatimaye kuondoana na adha zinazoweza kuwakumba ikiwemo
ukatili kutokana na utegemezi.
Uzinduzi
huo umeenda pamoja na Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga
Ukatili wa Kijinsia Duniani, yaliyoanza Novemba 25,2016 hadi leo Disemba
10,2016.
Na BMGHabari
Mgeni
rasmi ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mwanza, Kiteto Zawadi
Koshuma, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe,
uliotayarishwa na wanawake wajasiriamali kutoka Shirika la Sauti ya
Wanawake lililopo Ukerewe mkoani Mwanza.
Shirika
hilo limefanikiwa kwenye usindikaji wa bidhaa za kilimo ikiwemo
mbogamboga na matunda kwa msaada wa Shirika la Akina Mama Lishe la
Tanzania Entrepreneurs Development and Advocacy Organization TEDA.
Akina
mama wajasiriamali mkoani Mwanza wakimsikiliza mgeni rasmi, Mbunge wa
Viti Maalumu mkoani Mwanza, Kiteto Zawadi Koshuma, wakati akizindua Unga
wa Viazi Lishe hii leo Jijini Mwanza.
Koshuma
amewahimiza akina mama kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda
ikiwemo viazi lishe kwani soko lake ni kubwa ikizingatiwa kwamba viazi
hivyo vinatengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo vitafunwa. Amewashauri
kuzingatia suala la usindikaji wa mazao yao ili kuvutia zaidi soko la
ndani na nje ya nchi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Kombe Danty, akizungumza kwenye uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe mkoani Mwanza.
Pudentia
Ngereza ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika la Sauti ya Mwanamke kutoka
Ukerewe (Pia diwani Viti Maalumu Ukerewe), akizungumza wakati wa
uzinduzi wa unga wa viazi lishe unaozalishwa na shirika hilo.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora nchini ADLG, Jimmy Luhende,
akizungumzia ubora wa matumizi ya viazi lishe wakati akinunua unga wa
viazi hivyo baada ya kuzinduliwa rasmi hii leo mkoani Mwanza.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye
makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akitoa maelekezo kwa mgeni
rasmi kuhusiana na mbogamboga na matunda zinazozaliwa na taasisi yake.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye
makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akonesha bidhaa
zinazozalishwa na taasisi hiyo ambapo mteja hujipatia hoho, nyanya,
pilipili, chainizi, kabichi, karoti, bamia, mchicha, vitunguu,
tangawizi, mchaichai, karanga, kisamvu, sukuma wiki, vitunguu swaumu,
nyanya chungu na majani ya kunde ambapo kwa pamoja huuzwa kwa bei nafuu.
Aneth
Shosha ambaye ni Mratibu/Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media
Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akonesha bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa na taasisi hiyo ambayo pia imekuwa ikiwaunganisha
wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.
Simon
Nkwabe Ng'wanakilala ambaye ni msaidizi katika Taasisi ya Agri-Busness
Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akonesha bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa na taasisi hiyo ambayo pia imekuwa ikiwaunganisha
wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.
Mgeni
Rasmi amepokea zawadi ya vitafunwa zilivyotengezwa na Unga wa Viazi
Lishe kutoka Shirika la Sauti ya Wanawake kutoka Ukerewe mkoani Mwanza.
Mgeni rasmi akiwa pamoja na wageni kutoka taasisi na mashirika mbalimbali kwenye picha ya pamoja.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Ama Bonyeza hapo chini.
SHARE
No comments:
Post a Comment