Wafanyakazi wa TBL wakipanda miti katika moja ya kampeni ya upandaji miti
Kiwanda cha TBL cha Mwanza kimeunga mkono kampeni
ya kupanda miti inayoendelea mkoani Mwanza ambapo kimetoa miche 2,000
ya miti pia wafanyakazi wake wameungana na viongozi wa serikali na
wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali
kupanda miti katika eneo la Chuo cha Uvuvi .
Meneja Mwandamizi wa TBL,Mwanza,Joseph Malibe, alisema kuwa kampuni imeunga mkono jitihada hizi
ikiwa ni moja ya utekelezaji malengo ya kampuni ya kulipa suala la
mazingira kipaumbele popote inapofanyia biashara zake pia inayo sera ya
sera ya wafanyakazi kutumia muda wao kwa ajili ya kazi za kijamii.
“Tunafurahi
kushiriki katika tukio hili la kupanda miti lililoandaliwa na taasisi
ya mazingira ya Tanzania Environmental Conservation Organization (TECO)
kwa kuwa linaendana na mtazamo wetu wa kutunza mazingira na vyanzo vya
maji”.Alisema Joseph Malibe.
Alisema
kuwa TBL itaendelea kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira na
vyanzo vya maji popote inapoendeshea biashara zake ikiwemo kufanya
uzalishaji usio na athari kwa mazingira.
Malibe
alisema uzalishaji wa kutumia nishati mbadala tayari unatekelezwa
katika viwanda mbalimbali vya TBL “Hapa Mwanza tumeanza kufanya
uzalishaji kwa kutumia mitambo inayotumia nishati inayotokana na mashudu
ya pamba na pumba za mpunga na katika kiwanda cha Mbeya kimeanza
kufanya uzalishaji kwa kutumia umeme wa nishati ya jua”.
Alimalizia
kwa kutoa wito kwa watanzania wote kujenga utamaduni wa kutunza
mazingira ili kupunguza athari kubwa zinazoendelea kujitokeza sehemu
mbalimbali duniani kutokana na uharibifu wa mazingira.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment