TRA

TRA

Tuesday, March 28, 2017

Rouhani kukutana na Putin mjini Moscow

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
RAIS wa Iran Hassan Rouhani anafanya ziara nchini Urusi kwa mazunguzo yanayotarajiwa kujikita katika mahusiano ya kiuchumi na mzozo wa Syria. Rouhani amepangiwa kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin katika ikulu ya Kremlin leo. 

Wakati alipokutana na waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medbedev hapo jana, Rouhani alisifu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na kusema hatua zinazochukuliwa na Urusi na Iran zitasaidia kuimarisha amani na uthabiti katika eneo hilo na ulimwenguni kote.
            Rais wa Urusi, Vladmir Putin

Urusi, Uturuki na Iran zimesaidia kuafiwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosaidia kupunguza uhasama Syria na kuandaa duru mbili za mazungumzo ya amani mjini Astana, Kazakhstan. 

Urusi na Iran zimemuunga mkono kwa dhati rais wa Syria Bashar al Assad katika mzozo wa miaka sita, lakini Uturuki imewaunga mkono wapinzani.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger