Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Bariadi mkoani Simiyu-Picha zote kwa hisani ya Simiyu News blog
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Bariadi mkoani Simiyu
wakiandamana katikati ya barabara kuu ya Bariadi-Lamadi, mjini Bariadi
wakishinikiza kurudishwa Mkuu wa shule yao ambaye alikuwa amepewa
uhamisho Deus Toga, ambapo alikuwa amepelekwa shule ya sekondari Giriku
na kuletewa Mkuu wa shule mwingine Paul Lutema ambaye walimkataa.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi wakiandamana katikati ya barabara kuu ya Bariadi-Lamadi
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano hayo
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano hayo.
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakimkamata
mmoja wa wanafunzi wakati wa maanadamano hayo, ambapo walimkamata na
kumuweka kwenye gari la polisi.
Askari wengine akimkimbiza mwanafunzi ili kumkamata
Akari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwa katika
eneo la shule ya sekondari Bariadi, kuhakikisha wanafunzi wanaingia
darasani ili wasiendeleze maandamano.
Walimu wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu, wakiwatuliza wanafunzi wa shule hiyo wasiandamane tena, baada ya
kurudishwa na askari wa FFU kwa mabomu ya machozi kutoka katikati ya
barabara kuu ya Bariadi-Lamadi walipokuwa wakiandamana kwenda ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kupinga uhamisho wa Mkuu wao wa
shule.
Mwanafunzi akiwa amebebwa na wenzake baada ya kupoteza fahamu kutokana
na kupigwa na mabomu ya machozi, wakati wakiwa katika maandamano kwenda
ofisi ya mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kupinga uhamisho wa Mkuu
wao wa shule.
Mwanafunzi akiwa amepoteza fahamu
Wanafunzi wakiwa wamebeba mabango
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi
Festo Kiswaga, akiangalia mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanafunzi hao,
alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwatuliza, na kusikiliza madai yao
na kuamua mwalimu huyo kurejeshwa shuleni hapo.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi
Festo Kiswaga, akiangalia mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanafunzi hao
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akiwatuliza wanafunzi hao
Wanafunzi hao wakiwa wanaandamana, barabara kuu ya bariadi-Lamadi
****
ZAIDI ya Wanafunzi 600 wa shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo katika
halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga
barabara kuu ya Bariadi –Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule
hiyo Deus Toga.
Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa
halmashauri,lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi la polisi
kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo.
Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabara hiyo waliamua
kuandamana tena kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa jambo
lililoshindikana pia baada ya askari hao kuwazuia tena eneo la Hospitali
teule ya mkoa (Somanda).
Baada ya hali hiyo wanafunzi hao ambao ni kidato cha kwanza hadi cha
sita waliamua kukaa katikati ya barabara huku wakiimbanyimbo za
kushinikiza kuwa hawamtaki mwalimu Paul Lutema ambaye alikuwa
amepelekwa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
“Hatumtaki mwalimu Lutema……tunamtaka mwalimu wetu Toga…..hatumtaki Lutema……Tunamtaka mwalimu Toga”
Wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali za kumkataa mwalimu
Lutema na kumtaka mwalimu Deus Toga wanafunzi hao walianza kuwarushia
mawe askari hao wakitaka wasiwazuie kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa.
Baada ya hali hiyo askari wa jeshi la polisi walianza kutumia mabomu ya
machozi kuwatawanya wanafunzi hao huku wakiwafukuza kurejea katika eneo
la shule ambapo baadhi yao walikamatwa na kupigwa virungu na kuwekwa
ndani ya magari ya polisi hadi kupelekwa kituo cha polisi Bariadi huku
wengine wakipoteza fahamu.
“Tangu mwalimu huyu kafika shuleni hapa ufauru umeongezeka na migogoro
ya shule iliyokuwepo haipo tena,na duka la shule lilikuwa limefungwa
kutokana na migogoro ya walimu lakini toka amekuja hiyo migogoro
imekwisha na duka linafanya kazi’’,alisema Justine Mshana.
Hata hivyo Kaimu Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya
Bariadi Festo Kiswaga alifika katika shule hiyo na kusikiliza madai yao
na kuamua mwalimu huyo kurejeshwa shuleni hapo.
SHARE
No comments:
Post a Comment