Uchunguzi wa bunge la Marekani usioegemea upande wa chama chochote,
umeonyesha kuwa mpango wa bima ya afya unaopendekezwa na warepublican na
kuungwa mkono na Rais Donald Trump, utawaacha wamarekani wapatao
milioni 14 bila bima ya matabibu ifikapo mwaka ujao. Lakini pia ripoti
hiyo imeonyesha kuwa kuidhinishwa kwa mpango huo kutapunguza nakisi ya
dola bilioni 337 katika bajeti ya serikali katika muongo ujao, kiwango
ambacho ni kidogo kwa kuzingatia ukubwa wa bajeti ya Marekani. Hali
kadhalika, ripoti hiyo imesema gharama kwa mtu anayechukuwa bima ya afya
itaongezeka kwa asilimia kati ya 15 na 20 mwaka 2018 na 2019, kwa
sababu sheria hiyo inaondoa adhabu kwa watu wasionunua bima ya afya,
ikimaanisha kuwa watu wachache ndio watakaojitokeza kuichukua bima hiyo.
Kiongozi wa wademocrat katika Baraza la Seneti Chuck Schumer amesema
ripoti hiyo ni ishara tosha kwa warepublican kuachana na mpango huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment