Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha kutekwa
nyara kwa wafanyakazi wawili wa Umoja wa Umoja wa Mataifa katika jimbo
la Kasai katikati mwa nchi hiyo. Msemaji wa serikali Lambert Mende
amesema mmarekani Michael Sharp na msweden Zahida Katalan walichukuliwa
mateka pamoja na raia wanne wa Kongo; madereva watatu na mkalimani,
walipokuwa wakisafiri kwa pikipiki katikati mwa jimbo la Kasai.
Haijabainishwa lini utekaji nyara huo ulifanyika, na waliochukuwa watu
hao bado hawajatangaza chochote. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, umesema unafanya kila
linalowezekana kujua walipo watu hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment