Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahirisha safari yake mjini
Washington hadi mwishoni mwa juma, kutokana na hali mbaya ya hewa katika
mwambao wa Mashariki mwa Marekani. Bi Merkel alitarajiwa kufanya
mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani hii leo. Akizungumza na
mameneja wa biashara mjini Munich kabla ya ziara hiyo, Kansela Merkel
amesema biashara huria ni kitu muhimu baina ya Ujerumani na Marekani.
Ujerumani inataka kupata ufafanuzi, baada ya Rais Trump kutamka mara kwa
mara,kwamba anaazimia kuweka sera za kulinda biashara na ajira za
wamarekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment