Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Bwire Ndazi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board)
Peter Maduki akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi wa rasmi wa Bodi
hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt.
Bwire Ndazi.
Kaimu
Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi akizungumza mara baada ya Bodi ya
uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board)
Peter Maduki (kushoto).
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi
taarifa ya utekelezaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA) Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Peter Maduki wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimsikiliza
mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VET – Board) kupitia Bakwata Suleiman Lolila (kulia) mara baada ya
kuzindua Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti Mpya
wa Bodi hiyo Peter Maduki (katikati).
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi na Kushoto ni Mwenyekiti Mpya wa
Bodi, Peter Maduki.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
Na: Frank Shija, MAELEZO.
BODI
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara
moja kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa
ukisuasua kwa muda mrefu huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya
utekelezaji miradi hiyo.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi
Mpya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam.
Profesa
Ndalichako ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa
utekelezaji wa miradi hiyo huku kukiwa na shilingi takribani bilioni
14.5 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya
kazi hizo.
“Inasikitisha
kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017,
huku karibu miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile
tu ya kujengea uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji
kubwa kwa sasa.”Alisema Profesa Ndalichako.
Ndalichako
ameongeza kuwa Bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja
na kuwachukulia hatua watendaji watakao bainiuka kuhusika katika
ucheleweshaji wa kuanza kwa miradi hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki amempongeza Waziri
Ndalichako kwa kuwa muwazi katika kuelezea kutolridhishwa na udhaifu
katika utendaji kwa baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuahidi
kushughulikia suala hili huku akiwataka wajisahihishe badala ya kusubiri
kuwajibishwa.
“Mhe
Waziri, maelekezo yako tumeyapokea, nikuahidi tu kuwa mimi pamoja na
timu yangu tutayafanyika kazi, ni nisememe wazi tupo tayari kushirikiana
nawe wakati wowote,” alisema Mduki.
Awali
akisoma maelezo mafupi kuhusu Bodi ya Mamlaka hiyo wakati, Kaimu Mkuu wa
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Dkt. Bwire Ndazi
amebainisha changamoto kadhaa katika eneo hili la utoaji wa elimu na
mafunzo ya ufundi stadi kuwa ni pamoja na uwezo mdogo wa VETA na wadau
katika kufikia mahitaji ya elimu na mafunzo ya ufundi akitolea mfano
kuwa watu wanaohitaji kujiunga na mafunzo wanakadiriwa kuwa laki sita
kwa mwaka, uwezo wa vyuo vyote vya VETA, VYA Serikali na binafsi ni kati
ya 125,000 tu kwa mwaka.
Bodi
iliyomaliza muda wake iliundwa Agosti 2011 na kumaliza muda wake
kisheria Agosti 2014, na baadaye kuongezewa muda hadi desemba 2016
alipoteuliwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe 10
kutoka maeneo ya ujuzi mbalimbali.
SHARE
No comments:
Post a Comment