Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Harrisson Mwakyembe amesema
Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka hivyo, basi Serikali
haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha
Wanasheria.
Amesema
kuwaingiza wanachama ambao wana nasaba za siasa au viongozi wa vyama
vya siasa ndani ya TLS ni kuruhusu mgongano wa maslahi na yeye kama
mwanasheria hawezi kulikubali jambo hilo. DKt Mwakyembe alikuwa
akizungumza hayo na ugeni wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
uliokuja kumtembelea Ofisini kwake mjini Dodoma ukiongozwa na Rais wao
Bw. John Seka
“Kama
Wizara hatujui mwelekeo wa TLS kwa sasa, hatuwezi kuiacha TLS
ikijiingiza katika siasa halafu tukawaangalia tu. Hatuna nia ya
kuitawala TLS, ila tunawajibika kuwasimamia kwa kuwa Sheria yenu iko
chini yetu, mkiharibu kwa lolote Wizara ndio yenye wajibu wa kuwatolea
maelezo, katika hilo mnalotaka kulifanya sasa kuna mgongano wa maslahi,
je nyinyi kama wanasheria hamkuliona au hamlioni?, alisema Mhe
Mwakyembe.
Alisema
Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya
siasa ila ni lazima wafahamu kwamba viongozi wanaowachagua ambao ndio
watakaobeba sura ya TLS na mwelekeo mzima wa chama kama wanataaluma
hawapaswi kuwa na nasaba za kisiasa ili kuepusha mgongano wa maslahi
unapoweza kujitokeza.
“Serikali
haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila
tatizo linakuja pale mnapotaka kuchagua viongozi ambao tayari wanazo
kofia mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vya siasa, hao ndio
watakaobeba sura na mtazamo au mwelekeo wenu hapo hatuwezi kukubali kwa
kuwa watatenganishaje uongozi wao katika chama husika na uongozi wao
ndani ya TLS, huo sasa ndio mgongano wa maslahi alisema Dkt. Mwakyembe
na kuongeza kuwa ndio maana mwanasheria yoyote akiingia katika utumishi
wa umma uwakili wa kujitegemea anauweka pembeni ili kuepuka mgongano wa
maslahi.”
Alisema
TLS sasa imekuwa na haihitaji muangalizi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma
nchi ilipopata uhuru, kwani ina wasomi wengi na vijana wengi wamekuwa
wanachama pia na kwa hiyo ni bora tuifute hii Sheria yenu na tuwape
mwanya mkajisajili kama NGO ambako kiongozi yeyote wa chama cha siasa
anaweza kuwa kiongozi wao.
Amewataka
wafahamu kuwa dhamira ya Serikali ni njema huku ikizingatiwa kwamba
Sheria kama zilizvyo taaluma nyingine nchini bado zinahitaji uangalizi
hasa ukizingatia uingiaji wa nchi katika utengamano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Akizungumza
katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Sifuni Mchome alisema
kila taaluma ina namna ya uangalizi wake. alisema kama wanasheria lazima
kuhakikisha hatutoi vipaumbele kwa siasa kama zilivyo fani nyingine
nchini. Alitaka wajiulize kama kweli hawauoni mgongano wa maslahi huku
wakizingatia kuwa wanapaswa kuhudumia jamii ya watanzania bila ya
kuwabagua.
“Kama
wanasheria lazima tuhakikishe hatutoi vipaumbele kwa siasa kama zilivyo
fani nyingine, jiulizeni kama kweli hamlioni jmabo hilo kama ni kikwazo
huku mkizingatia kuwa tunatakiwa kuhudumia jamii bila ya kuwabagua sasa
tukijiingiza katika siasa tutaihudumiaje jamii husika? TLS
kutojihusisha na siasa ni miongoni mwa kanuni za kutuimarisha kama
wanataaluma,”alisema Prof Mchome
Alisema
Wizara ipo kuiangalia TLS, na ndicho ilichofanya, imewastua jamani
mnaenda wapi? tunataka muende katika mstari sahihi, nawataka mjiulize
hivi kweli kamati ya uchaguzi haijaona kama kuna mgongano wamaslahi
hapo?
“Tupo
hapa kuwangaalia, na ndicho tulichofanya, tumewashtua jamani mnanenda
wapi? Hatuna nia mbaya ila tunawataka muwe katika mstari, hivi kweli
kamati ya uchaguzi haijaona kama kuna mgongano wa maslahi hapo?
Alisema
Serikali haitasita kuchukua hatua ya kuifuta Sheria ya TLS kama chama
hicho kitaendelea na msimamo wa kujihusisha na masuala ya siasa au
kiuharakati chama hicho katika siasa na hawana budi zaidi ya kuangalia
namna wanavyoweza kujikwamua katika hilo.
Kama
hamuwezi kuendeleza misingi ya kitaaluma ya kutojihusisha na siasa au
vyama vya siasa basi serikali haitakuwa na namna zaidi ya kuifuta sheria
ya TLS na TLS ya sasa itabidi ikajisajili kama NGO ili iendeleze
harakati zake na Serikali itaunda sheria nyingine itakayoanzisha chombo
kitakachosimamia misingi ya kitaaluma.
Naye
Rais wa TLS bw. John Seka akizungumza katika kikao hicho alisema
ameelewa maoni ya Serikali na kwamba kuonekama kwa TLS kama inajiingiza
katika siasa kunatokana na wanachama ambao ni viongozi au wanachama
katika vyama vya siasa ambao kwa sasa wanataka uongozi wa chama hicho.
Ameiahidi
serikali kuwa TLS itaendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya
kuanzishwa kwake ambapo pia haina mpango wakuwa chama cha siasa au chama
cha kiharakati na hivyo kuiomba Serikali kuifanyia marekesbisho Sheria
yake ili iweze kukabili changamoto inazokabilian nazo kama ilivyotokea
sasa ambapo mwanachama ni kiongozi wa chama cha siasa na hivyo kuwa na
haki ya kuomba uongozi wa TLS
Amesema
anaiomba wizara na watendaji wake kuendelea katika mazunguimzo na TLS
ili kuweza kuhakikisha inatekeleza na kufikia malengo yote ya kuanzishwa
kwake huku akiahidi kuwa siku zote TLS haitogwanyika, itasimamia na
kuongoza wanachama wake ipasavyo na kuhakikisha misingi na maadili ya
taaluma ya sheria inazingatiwa ili TLS iendelee kubaki kama ilivyo sasa
na kutokupendelea upande wowote.
SHARE
No comments:
Post a Comment