Mkurugenzi Mtendaji wa
Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios (kulia), akigongesha soda ya Coca-Cola
na viongozi wengine wa kampuni hiyo kuashiria uzinduzi wa muonekano mpya
wa chupa ya kinywaji hicho mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki. Wengine
katika picha (kutoka kushoto) ni David Karamagi – Meneja Mkazi wa
Coca-Cola Tanzania, Nalaka Hettiaratchchi – Mkurugenzi wa Mauzo wa
Coca-Cola Kwanza na Gary Pay – Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza Mbeya.
Sambamba na uzinduzi wa muonekano mpya, Kampuni ya Coca-Cola
imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa zake mkoani Mbeya ambapo
imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia teknolojia ya kisasa katika
kiwanda chake kilichopo Mbeya. Picha zote na Mr. Pengo – MMG-MBEYA.
Wageni waalikwa waliofika kusherekea muonekano mpya wa kinywaji cha Coca-Cola.
—
*Yafunga mitambo ya uzalishaji ya kisasa, boresha huduma za usambazaji wa bidhaa zake
Kampuni ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa
zake mkoani Mbeya ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia
teknolojia ya kisasa katika kiwanda chake kilichopo Mbeya , sambamba na
kununua malori mapya kwa ajili ya kurahisisha usambazaji lengo kubwa
likiwa ni kuhakikisha bidhaa zake zinapatikana katika kila kona ya mkoa
huo na maeneo mengine yote ya Nyanda za Juu Kusini.
Kutokana na mkakati wake huu
wenye mwelekeo wa kupanua soko lake, kampuni jumamosi hii imefanya
tafrija maalum ya kusherehekea mafanikio haya iliyofanyika katika hoteli
ya Tughimbe na kuwajumuisha wadau zaidi ya 300 kutoka sekta mbalimbali
mkoani humo, wakiwemo wafanyabiashara, mawakala wa usambazaji vinywaji
na wanamichezo kutoka klabu ya Mbeya FC ambayo inadhaminiwa na
Coca-Cola.
Akiongea wakati wa hafla hiyo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios, alisema upanuzi
na kufunga mitambo ya kisasa zaidi katika kiwanda cha Coca-Cola mkoani
Mbeya umefanyika wakati muafaka ambapo umeenda sambamba na mkakati wa
kujiiimarisha zaidi katika soko la Mkoa huo na maeneo yote ya Nyanda za
Juu Kusini na kuhakikisha bidhaa zake zinapatikana kila mahali na wakati
wowote lengo likiwa na kuwawezesha wakazi wa Mbeya kufurahia ladha
murua ya kinywaji cha Coca-Cola na bidhaa nyingine zinazozalishwa na
kampuni.
“Kampuni ya Coca- Cola inayo
historia ya kuwepo mkoani hapa kwa muda mrefu, na tumeona ni vyema
tukawashirikisha katika mkakati wetu wa mafanikio wenye lengo la
kuongeza tija na ufanisi, ambapo tumeboresha kiwanda chetu na pia
tumejipanga kusambaza bidhaa zetu kuhakikisha zinawafikia wananchi kwa
urahisi na mkakati huu tutautekeleza katika mikoa yote vilipo viwanda
vyetu”. Alisema Bwana Gadzios.
Kwa upande wake, Mkuu wa kiwanda
hicho cha Mbeya, Gary Pay, alieleza kuwa kiwanda hicho kimefanyiwa
ukarabati mkubwa na kufungwa mitambo inayotumia teknlojia ya kisasa ya
uzalishaji vinywaji, kujenga mabohari ya kisasa na kununua malori
makubwa ya kurahisisha usambazaji bidhaa zake kwa wateja.
Bwana Pay alisema uwepo wa
kiwanda hicho umetoa ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa
moja kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa kampuni imekuwa
mstari wa mbele kutekeleza miradi ya kusaidia jamii, baadhi yake ikiwa
ni kutoa msaada wa madawati kwa shule za serikali na udhamini wa timu ya
mchezo wa soka ya Mbeya FC.
Alimalizia kwa kusema kuwa
kampuni itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na
changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii ambapo katika kipindi cha
mwaka huu kampuni imedhamiria kutoa msaada wa madawati 1,000 katika
shule za serikali za mkoa humo.
SHARE
No comments:
Post a Comment