Katika kuwapunguzia watanzania
mzigo wa gharama za vifurushi vya intaneti kampuni ya mawasiliano ya simu ya
Halotel imetangaza kuboresha vifurushi vyake vya intaneti na kuongeza kiwango kulingana
na mahitaji ya wateja.
Akizungumzia juu ya maboresho hayo, Kaimu Mkurugenzi
wa kampuni hiyo Bw. Lui Van Dai, amebainisha kuwa azimio hilo limekuja baada ya
kusikia kilio cha watanzania kuhusu gharama za intaneti kuongezeka lakini
vifurushi vikiendelea kushuka kila kukicha.
“Tumesikia kilio cha Watanzania ambao wameendelea
kulalamikia gharama za mawasiliano kuendelea kupanda siku hadi siku kitu
ambacho kinaathiri matumizi yao. Maboresho haya yanalenga kuwapatia vifurushi
zaidi kwa kiasi kidogo cha fedha ambacho kinaendana na mahitaji ya kila mteja.”
Alisema Dai.
“Tunatambua teknolojia ya mawasiliano imekua kwa
kiasi kikubwa na inatumika katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Sekta hii imekuwa ni kiungo kizuri katika upashanaji wa habari hususani
mitandao ya kijamii ambayo ndio njia rahisi na ya haraka kuwafikia watu. Hivyo
basi, maboresho haya yanalenga kuendelea kuwapatia Watanzania muda zaidi wa
kuendelea kuungana na jamii kwa kufurahia vifurushi vikubwa kwa kiasi kidogo
cha fedha.” Aliongezea Mkurugenzi huyo.
Ameendelea kufafanua zaidi kuwa licha ya kufanya
maboresho hayo, Halotel imefanya uwekezaji mkubwa katika teknolojia ya
mawasiliano kwani mbali na kupunguza gharama hizo wanawahakikishia Watanzania
kuwa huduma zao ni za uhakika na zinapatikana kila kona ya nchi.
“Hadi sasa tumeweza kuvifikia vijiji zaidi ya 3000
nchi nzima ambapo kitakwimu ni sawa na kusema tumesambaa Tanzania kwa asilimia
95% hadi hivi sasa. Pia tumeunganisha mtandao wetu kwa zaidi ya Kilomita 20,000
za mkongo wa mawasiliano. Hii inafanya huduma zetu kuwa ni za uhakika na
kutufanya kinara katika kuyafikia maeneo mengi zaidi kuliko mtandao wowote
nchini.” Aliendelea kuelezea zaidi Dai.
“Kwa hali ilivyo ngumu sasa tumeboresha zaidi
vifurushi vyetu ambapo kwa Shilingi 499, mteja atapata MB 200 pamoja na dakika
za kupiga simu. Kiwango hiko ni kikubwa zaidi cha MB kinachotolewa
ukilinganisha ni mitandao mingine kwa zaidi ya 100%. Kwa Shilingi 1000, mteja
anaweza kupata MB 450, pamoja na vifurushi vingine vingi. Hivyo nawasihi
Watanzania kuendelea kujiunga na Halotel ili waendelee kufurahia huduma zetu
kwa gharama nafuu.” Alihitimisha Bw. Dai.
Kampuni ya Halotel licha ya kuwekeza zaidi katika
mfumo wa mawasiliano ya simu pia inatoa huduma kwa gharama nafuu zaidi kwa
mamilioni ya Watanzania. Dhumuni kuu ni kuwapunguzia gharama na kuwawezesha
kuendelea kufurahia huduma za intaneti zenye uhakika zaidi.
SHARE
No comments:
Post a Comment