Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linatiwa wasiwasi na
ripoti za mateso na kutoweka kwa watu vinavyoripotiwa nchini Burundi,
lakini limepuuza miito ya mashirika ya haki za binadamu kutaka nchi hiyo
iwekewe vikwazo. Tangazo lililoandaliwa na Ufaransa kuhusu nchi hiyo
limepitishwa kwa kauli moja, baada ya upinzani wa Urusi, China na Misri
ambazo zinapinga vikwazo dhidi ya Burundi. Katika tangazo hilo baraza
limesema hali kwa ujumla ni ya utulivu nchini Burundi, na kuongeza
lakini kuwa idadi kubwa ya watu wanaendelea kuikimbia nchi hiyo. Wakati
huo huo serikali ya Burundi imetangaza ugonjwa wa Malaria kuwa jana la
kitaifa, ikisema maradhi hayo yameuwa watu zaidi ya 700 mwaka huu pekee.
Waziri wa afya wa nchi hiyo Josiane Nijimbere amesema idadi ya vifo ni
ya kutisha, na kuongeza kuwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri
chini ya miaka mitano ndio wanaokabiliwa na kitisho kikubwa zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment