Benki ya
EFC Tanzania Microfinance Bank ltd leo imezindua huduma mpya kwa wateja
wake ya mtandao wa kibiashara wenye lengo la kuboresha mawasiliano kati
ya wateja na benki itakayosaidia kurahisisha utoaji huduma hasa katika
shuguli zao za ukopeshaji, ambapo Benki hiyo inaamini mawasailiano
mazuri na mteja ni jambo muhimu katika kipindi hichi ambapo benki inakua
kwa kasi.Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika Makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo
maeneo ya Victoria Barabara mpya ya Bagamoyo Jijini Dar es slaam
Mkurugenzi mtendaji Bwana Bas Nierop amesema
EFC sasa ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha inaongeza matawi yake Dar es
salaam na Mikoani ili kuweza kuwasogezea wananchi huduma za kibenki na
mikopo kwa ukaribu zaidi.
Aidha
bwana Nierop ameongeza kuwa miaka sita sasa imepita tangu EFC ianze
kutoa huduma zake kama taasisi ya mikopo na imekuwa ikijiendesha vizuri
kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja wake kiasi kwamba wameiona ipo haja
ya kutanua wigo wa kibiashara na kuwa Benki kamili yenye uwezo wa kutoa
mikopo kwa wajasiliamali na kuwahudumia kibenki zaidi, ambapo wataweza
kutoa na kuhifadhi fedha kwa usalama zaidi nakunufaika
Nae
Mkurugenzi wa kitengo cha mikopo Bwana Robert Pascal amesema katika
kuboresha huduma zao Benki hiyo imeanzisha utaratibu wa kukutana na
wateja wake mara kwa mara ili kuweza kusikiliza na kutatua changamoto
zinazowakabili wateja wao na kuona namna bora ya kuboresha huduma zao
kwa wateja wao.Pia bwana Pascal kawasisitiza wateja kua waaminifu ili
kujenga mahusiano mazuri na benki.
Meneja
masoko wa Benki hiyo Bi Waheeda Mohamed amewataka wakazi wa Dar es
salaam kuchangamkia fursa ya kujiunga na benki yao kwani sasa benki hiyo
imeweza kupiga hatua na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo kwa
masharti nafuu ambayo hata Mwananchi wa kwaida anaweza kumudu.
SHARE
No comments:
Post a Comment