KUELEKEA
fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini
Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa na Mwenyekiti
Charles Hilal imeandaa wimbo wa pamoja utakaoimbwa na wasanii maarufu wa
muziki wa Bongo Fleva, Naseebb Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh ‘King Kiba'
pamoja na wasanii wengine. Wimbo huo wa pamoja ni maalum kwa ajili ya
kuhamasisha kampeni za kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri
wa miaka 17, Serengeti Boys itakayofanyika mwezi wa tano nchini Gabon
ambapo zitapatikana nchi nne zitakazokwenda kombe dunia la vijana nchini
India. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Charles Hilal amesema kuwa kwa pamoja
wimbo utakaowahusisha wasanii wengine mbalimbali utakuwa na lengo kuu
la kuhamasisha wananchi, wadau na wapenda michezo kuichangia timu hiyo
ya vijana kwa lengo la kuisaidia malengo waliyokuwa wameyafikia ya
kuipeleka timu hiyo kwenye fainali za kombe la Dunia nchini India. Hilal
amesema kuwa hatua hii ya kusaidia Serengeti Boys kutawajenga vijana
hawa kufanya vizuri katika michuano ya mataifa Afrika kwa vijana ikiw
ani pamoja na kupata kambi nje ya nchi na kuchgeza mechi kadhaa za
kirafiki kutoka nchini jirani lakini hata hivyo bado wanafikria kutafuta
mechi ya kirafiki itakayochezwa hapa hapa Jijini Dar es salaam ikiwa ni
kwa ajili ya kuwaaga kuelekea nchini Gabon. Mjumbe wa Kamati ya
Serengeti Boys, Maulid Kitenge amesema kwamba tayari ala za wimbo huo
zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote wametumiwa kwa ajili ya
kuingiza sauti, ili mara moja wimbo huo ukamilishwe na kuanza rasmi
kusaidia kampeni ya kuhamasisha Serengeti Boys.
“Tayari
wasanii Ali kiba na Diamond wameshakubali kurekodi nyimo hiyona
wameahidi kufanya haraka kuingiza sauti kwenye ala ambazo tumeshawatumia
na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almasi, Darasa na Vanesa Mdee
nao wataweka sauti zao,"amesema Kitenge.
Kiba na
Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha
Watanzania kwa pamoja ili kuichangia Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za
Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.
Katibu wa
Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Kitenge wa EFM Radio
na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice
Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu, yumo Mkurugenzi
wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan
Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na
Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.
Pia,
Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua kuanzia Bodi
ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa kwa lengo la
kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.
Mwenyekiti
wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya Serengeti Boys kueleka
kwnye kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 yatakayofanyika nchini
Gabon. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini Bw. Omary Singo
na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano
Mwenyekiti
wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akiwa pamoja na
Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge wakiwasikilizisha
waandishi ala za wimbo unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya kuhamasisha
kuichangia Serengeti Boys.
SHARE
No comments:
Post a Comment