Rais wa Urusi Vladmir Putin amepangiwa kukutana na kiongozi mwenzake
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Moscow hii leo kujadiliana kuhusu
vita vinavyoendelea nchini Syria pamoja na kuimarisha uhusiano wa
kibiashara kati ya nchi hizo mbili.Hayo ni kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na ikulu ya Kremlin.Urusi na Uturuki nchi ambazo zinaunga
mkono pande tafauti zinazopingana katika vita nchini Syria zimekuwa
zikijaribu kujenga upya mahusiano yao katika kipindi cha miezi ya hivi
karibuni baada ya ndege ya kivita ya Uturuki kudungua ndege ya kijeshi
ya Urusi katika anga ya mpaka wa Syria na Uturuki mwishoni mwa mwaka
2015. Mkutano huo unakuja baada ya rais Putin hapo jana kukutana na
waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kuzungumzia mgogoro huo wa
Syria na juhudi za kupambana na ugaidi wa Kimataifa na hasa kundi
linalojiita dola la Kiislamu
No comments:
Post a Comment