TRA

TRA

Friday, March 31, 2017

Ghasia zazuka ubalozi wa Uturuki, Brussels

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya katika ghasia zilizotokea mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Brussels, Ubelgiji jana. 

Rabsha hizo zimetokea wakati wafuasi na wapinzani wa Rais Recep Tayyip Erdogan waliposhambuliana. 

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, watu wanne wamejeruhiwa na Wakurdi watatu wamechomwa kisu na wafuasi wa Rais Erdogan kabla ya polisi kuingilia kati mzozo huo. Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel amelaani ghasia hizo akisema serikali ya Ubelgiji haitovumilia kabisa ghasia zinazotokana na kura ya maoni nchini Uturuki, yenye lengo la kumpa madaraka zaidi Rais Erdogan. Kura hiyo ya maoni itafanyika Aprili 16.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger