Serikali ya Rais Donald Trump imekata rufaa kuhusu uamuzi wa jaji wa
Marekani ambaye alizuia kwa muda usiojulikana utekelezaji wa marufuku ya
kusafiri iliyotangazwa na Rais Trump.
Rufaa hiyo ilikatwa jana, siku
moja baada ya Jaji wa Mahakama ya Jimbo la Hawaii, Derrick Watson
kutangaza pigo jingine kwa Trump, la kuwazuia watu kutoka nchi sita za
Kiislamu kutoingia Marekani.
Amri ya awali ya Rais Trump ilikuwa
inawazuia kwa siku 90 raia wa Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na
Yemen kuingia nchini Marekani na wakimbizi wote kwa angalau siku 120.
Amri ya awali ya rais ilikuwa inaijumuisha pia Iraq, lakini nchi hiyo
iliondolewa kwenye orodha hiyo. Rais Trump amesema pendekezo la kupiga
marufuku watu kusaifiri linahitajika ili kulinda usalama wa taifa hilo
na kuwaweka nje magaidi wanaokusudia kuwadhuru Wamarekani.
No comments:
Post a Comment