Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) leo mchana jiini Dar kuhusiana na maandalizi
ya tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kufanyika Aprili 16 mwaka huu
kwenye uwanja wa Taifa likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa
injili.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo jambo kwa
kina mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar leo
kuhusu maandalizi ya tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kufanyika
Aprili 16 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa likishirikisha waimbaji
mbalimbali wa muziki wa injili.
KAMATI
ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka chini ya mwenyekiti wake Alex Msama,
limeanza kutaja waimbaji wa nyimbo za injili watakaoshambulia ‘tamasha
la mwaka huu.
Mwimbaji
wa kwanza kutajwa na Kamati hiyo katika mkutano wake na waandishi
habari jijinin Dar es Salaam leo , ni Jesca Honole maarufu kama ‘Jesca
BM.’
Msama
amesema leo kwamba, mwimbaji huyo amepata bahati ya kipekee ya kuwa wa
kwanza na kwamba wengine watawekwa hadharani baada ya kupitishwa rasmi
na Kamati.
“Tunamshukuru
Mungu kwa sababu maandalizi ya Tamasha letu la Pasaka ambalo safari hii
linakuja kitofauti zaidi, waimbaji wameanza kupitishwa, ikiwa ni hatua
nzuri ya tukio hili la kimataifa,” alisema Msama na kuongeza.
‘Mwimbaji aliyebahatika kuwa wa kwanza kuthibitishwa ni Jesca Honoli maarufu kama ‘Jesca BM’, mmoja wa waimbaji mahiri kwa sasa.
Alisema
nguvu ya kuanza kutangaza waimbaji watakaohudumu katika Tamasha hilo
litakaloanzia Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam April 16, ni baada
ya kupata kibali rasmi cha tukio hilo.
Kuhusu
kibali, Msama ametoa shukrani kwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa
kutoa baraka kwa tukio hilo la kimataifa ambalo litatikisa katika mikoa
ipatayo mitano ya Tanzania bara.
Alisema,
baada ya Tamasha hilo kuzindiliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru,
jijini Dar es Salaam, litahamia Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma kabla ya
kutua katika mikoa mingine mitatu.
Alisema
mbali ya Tamasha hilo kubeba malengo yake ya msingi yakiwamo ya kueneza
neno la Mungu na kutumia sehemu ya mapato kufariji makundi maalumu,
safari hii litatumika kama jukwaa la kumuombea nch Rais John Pombe
Magufuli na nchi kwa ujumla.
SHARE
No comments:
Post a Comment