Meneja Uendelezaji wa Biashara kitengo cha Huduma za Ziada wa Halotel, James Kulwijira
(Katikati) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya HALO SAINI huduma hii
itamuwezesha mteja wa mtandao huo, ambae tayari amejiunga na huduma hiyo kutengeneza
ujumbe maalum kuhusu biashara yake na kila atakapo piga simu au kupigiwa,
mhusika atapata ujumbe maalum utakaomueleza kuhusu biashara husika ya Mteja wa
Halotel. Pamoja katika picha ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo (kushoto) na
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Ziada Caroline Majaliwa.
KUENDELEA kukua kwa teknolojia ya mawasiliano nchini kumeendelea kuwawezesha
watanzania kupata nafasi ya kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa
na mitandao ya simu, Mtandao wa simu wa Halotel umezindua huduma itakayo
wawezesha wateja wake ambao ni wafanya biashara kuweza kutangaza
biashara zao bure kwa kutumia huduma mpya iliyozinduliwa na kampuni hiyo
inayojulikana kama Halo SAINI.
huduma
hii inamuwezesha mteja wa mtandao huo, ambae tayari amejiunga na huduma
hiyo kutengeneza ujumbe maalum kuhusu biashara yake na kila atakapo
piga simu au kupigiwa, mhusika atapata ujumbe maalum utakaomueleza
kuhusu biashara husika ya Mteja wa Halotel.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha huduma za Ziada
wa Halotel, Caroline Majaliwa amesema kuwa mapinduzi hayo ya
kiteknolojia yatawawezesha mamilioni ya wafanya biashara wanao tumia
mtandao huo kuweza kutangaza biashara zao kwa wale wanao wapigia na hata
wanaopokea simu zao.
“Licha ya kuendelea kuwa na huduma nzuri za kuvutia, tumeendelea
kubuni na kuja na huduma zitakazo wawezesha wateja wetu kuendelea
kufurahia huduma zetu kadha wa kadha na sasa kuwawezesha kutangaza
biashara zao kwa watu wanao wapigia au kupokea simu zao, ambapo baada ya
kuwezesha huduma hiyo wataweza kupokea ujumbe maalum ambao atahitaji
yeye mwenyewe ufike kwa wateja wake”. Alisema Majaliwa
Aidha
Majaliwa aliongeza kuwa, ili mteja aweze kufurahia huduma hiyo
atatakiwa kutuma neno ON kwenda namba 15614 kujiunga, na kisha atapaswa
kutuma neno SAINI kisha ujumbe ambao anataka watu waupate pindi watu
watakapokuwa wakimpigia au yeye kuwapigia kwenda kwenye namba 15614.
Kwa
Upande wake, Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Stella Pius amesema licha
ya kuwawezesha wateja wao kuweza kutumia nafasi hiyo kutangaza biashara
zao, Amesema kuwa wameamua kuwazawadia wateja wao wote ambao
wameendelea kuwaunga mkono, kwa kuwawezesha kushinda zawadi mbalimbali
kila watakapokuwa wanaweka muda wa maongezi.
“Tunathamini
sana mchango wa wateja wetu na tumeamua nasi kuendelea kuwazawadia kwa
kuwawezesha kujishindia zawadi kem kem kila wanapoweka vocha za mtandao
wa Halotel. Kila Mteja wa Halotel atakapoweka vocha katika simu yake
atapokea ujumbe wenye namba ya bahati ambayo atatakiwa kuituma kwenda
namba 0901220004 na ataingia katika droo ambayo itamuwezesha kujishindia
zawadi ya muda wa Maongezi au Smartphone zitakazo kuwa zinatolewa kwa
siku, wiki na kila mwezi kwa washindi watano (5)” Alisema Pius na
kuongeza;
“Tutakuwa
tunachezesha droo kwa siku, wiki na kila mwezi na washindi
watajishindia muda wa maongezi wa hadi shilingi elfu 50000/= pamoja na
simu za Smartphone zenye teknolojia ya hali ya juu,” Hili linatuwezesha
sisi kuendelea kuthamini mchango wa wateja wetu ambao wameendelea
kutuunga mkono siku hadi siku, Alihitimisha Pius.
Pamoja
na huduma hizo, kampuni hiyo pia imeboresha huduma nyingine ambazo
zitawawezesha wateja wa mtandao huo, kuweza kusikiliza redio katika
maeneo mbalimbali yaliyo na mtandao wa Halotel, hata kama hakuna masafa
ya FM/AM ya radio hiyo, katika eneo husika. Huduma nyingine
iliyozinduliwa sambamba na huduma hizo ni pamoja na huduma ya Halosoka
ambayo itamuwezesha mteja wa mtandao huo kuweza kupata matokeo ya mpira
wa miguu papo hapo.
SHARE
No comments:
Post a Comment