Rais
mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa
akizindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete
Foundation (JMKF) ikiwa ni sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye
Hotel ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro Dar es Salaam leo. Kikwete ni
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.
Mwenyekiti
wa Taasisi hiyo, Jakaya Kikwete, alisema kuwa Taasisi hiyo pamoja na
mambo mengine itajihusisha na masuala ya Maendeleo ya Binadamu nchini,
Afrika na Duniani.
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa anapenda
kuendelea kufanya shughuli zinazosaidia kuleta maendeleo kwa watu na
jamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa
akizindua Taasisi yake ya Jakaya Kikwete (Jakaya Mrisho Kikwete
Foundation) alisema kuwa kwa muda mrefu amekua akipenda na kujihusisha
na shughuli mbalimbali za maendeleo ya watu na hivyo Taasisi yake
itamsaidia katika kufikia malengo yake.
“Nimetumia
muda wangu kwa ajili ya maendeleo ya watu, baada ya shule,
nilikitumikia Chama cha Mapinduzi(CCM), nilitumikia Jeshi na baadae
Serikali, kwangu Taasisi hii imekuwa chombo kitakachonisaidia kuendeleza
maono yangu na kutimiza ndoto zangu katika kuendelea kusaidia watu”
alisema Dkt. Kikwete.
Akiizungumzia
taasisi hiyo Kikwete alisema kuwa, Taasisi yake ina wajumbe 9 kutoka
sehemu mbalimbali duniani wenye nyadhifa na heshima kubwa katika nchi
zao.
Ameongeza
kuwa Taasisi hiyo imejikita kusaidia jamii katika maeneo makubwa manne,
maendeleo ya jamii hasa katika kujikita kuondoa umaskini, mabadiliko
ya hali ya nchi na kilimo kwa wakulima wadogo.
Pia Taasisi hiyo imejikita katika huduma za afya, kutokomeza malaria na afya ya mama na mtoto.
Maeneo
mengine ambayo Taasisi hiyo inajihusisha nayo ni ni elimu kwa vijana
ili kukuza vipaji vyao na kuwapa mafunzo kuhusu uongozi bora, usawa wa
kijinsia na namna ambavyo Serikali inavyotoa huduma kwa wananchi.
Aidha,
alisisitiza kuwa Taasisi yake itaisaidia Serikali, mashirika na Taasisi
mbalimbali ili kushirikiana kuwaletea maendeleo watanzania na watu
mbalimbali duniani.
Dkt.
Kikwete amewataja Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi yake kuwa ni
Balozi Ombeni Sefue aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Profesa Rwekaza
Mukandala Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa
Willium Mahalu Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Tabibu cha
Bugando.
Wengine
ni Balozi Mwanaidi Maajar aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza, Abubakar Bakhresa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni
ya Bakhresa, Genevieve Sangudi Mtaalamu wa Masuala ya kibishara ya
Kimataifa kutoka Marekani.
Pia
wapo Dato’ Sri Idris Jala, Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu nchini
Malyasia, Balozi Charles R. Stith aliyekuwa Balozi wa zamani wa
Marekani nchini Tanzania pamoja na Dkt. Carlos Lopes ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taaisi ya Mafunzo na Utafiti ya Umoja wa Mataifa
(UNITAR).
Taasisi
ya Maendeleo ya Jakaya Kikwete ilisajiliwa tarehe 17, Februari 2017, na
hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini kukutana tangu
kuanzishwa kwake.
Kikwete akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi yake ya JMKF
Jakaya
Kikwete akikumbatiana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo,
Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania, Charles Stith
Mwenyekiti
wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo,
Mfanyabiashara maarufu Mtanzania aishie Marekani, Genevieve Sangudi
Mwenyekiti
wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo
ya Wadhamini , Dato’ Sri Idris Jala, Waziri asiye na Wizara Maalumu
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (Pamendu) nchini humo.
Mwenyekiti wa JMKF, Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taasisi hiyo.
Jakaya akijadiliana jambo na Balozi Charles Stith
Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo.
Jakaya Kikwete akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Taasisi hiyo
Dato’ Sri Idris Jala kutoka Malaysia
Genevieve Sangudi kutoka Marekani
Mwanasheria Maarufu nchini, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar. Alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza 2006 na Marekani 2013
Daktari Bingwa wa Upasuasi, Profesa Wiliam Mahalu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara
Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni la SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa
Balozi wa zamani wa Marekani nchini, Charles Stith
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
SHARE
No comments:
Post a Comment