Mgeni
rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale
alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 pamoja na
kuzindua jarida maalum la kikosi hicho akiwa amelishika linaitwa
Uhodari.
Baadhi
ya wanajeshi wa kikosi cha 841kj wakionyesha ukakamavu wake kwa
kushindana kuvuta kamba ikiwa na lengo la kuburudisha wakati wa sherehe
za miaka 50 ya kikosi cha 841kj
Baadhi
ya vijana waliopo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi maarufu kama
operation Magufuli kujitolea katika kikosi cha 841kj mafinga nao
walikuwa miongoni mwa waliosherekea miaka 50 ya kikosi hicho.
Hili
ndio jengo linalojengwa kwa ajili ya kiwanda cha Kukoboa na kusaga
nafaka za kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga.
Na Fredy Mgunda,Mafinga
Kikosi
cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kimeanzisha kiwanda kwa ajili
ya kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha
jeshi hilo linajilisha na kupata mahitaji mengine kupitia uzalishaji
mali.
Akizungumza
kaimu kamanda wa kikosi cha 841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika
maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 /
1967 kikiwa na lengo la kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa na serikali ya viwanda
kwa kuanza kujenga kiwanda cha nafaka na mifugo ambacho kitatoa ajira wa
watu wengi na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja na kuimalisha
ulinzi kutokana na majukumu waliyonayo.
Nkya
alisema kuwa kikosi cha 841kj kj mafinga kimeamua kujenga kiwanda hicho
ambacho kitakuwa kinaendeshwa kibiashara ili kukuza ajira na pato la
taifa.
“Hapa
kikosini tunalima na kufuga mifugo ya aina mbalimbali kwa wingi na kwa
kiwango kinachotakiwa kukidhi soko ili kuonyesha kuwa kikosi cha jeshi
la kujenga taifa 841kj mafinga kinakuwa mfano wa kuigwa na kukidhi haja
ya kuanzishwa kwa kikosi hicho”.alisema Nkya
Captain
Nkya alisema Sasa hivi Jeshi la kujenga taifa kikosi cha 841kj kimekuwa
kikosi cha Kisasa nachenye wasomi wengi wanaweza kusaidia kubuni vitu
vingi vyenye faida ya kulisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake
kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika
shughuli nyingine za kijamii.
“Tumefungua
kiwanda ni lazima sasa kuongeza uzalishaji kwa lengo la kuja
kuipunguzia serikali gharama za kukihudumia kikosi cha 841kj mafinga
ukiangalia tunaeneo kubwa na tunanguvu kazi hivyo ni lazima tulime na
kufuga kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuli anataka jeshi la kujenga taifa lirudi kujitegemea”.alisema Nkya
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu
Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50
kwa kuwa kudumu huko kwa kikosi hicho ni hatua kubwa sana katika ujenzi
wa taifa.
Chale
alikitaka kikosi cha 841kj kurudisha uzalendo kama zamani ili kuendelea
kuzalisha chakula kwa wingi kama zamani kwa saizi kikosi hicho kin alima
eneo dogo sana kitu kinachochangia kuipa serikali wakati mgumu wa
kikihudumia kikosi hicho.
“Nimetembea
eneo kubwa sana leo lakini nimeona eneo la uzalishaji ni dogo sana
hivyo mnahitaji kuongeza uzalishaji ili kuisadia serikali kuzalisha
chakula kwa wingi nyie mna nguvu kazi hapa lakini bado sijaona mkiitumia
ipasavyo”.alisema Chale
Aidha
Chale alikipongeza kikosi hicho cha 841kj mafinga kwa kumuunga mkono
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa
kuanza ujenzi wa kiwanda ambacho kitaongeza ajira,uzalishaji wa bidhaa
za chakula na kukuza uchumi wa nchi kutokana na uzalishaji wake.
“Nichukue
fursa hii kuwapongeza kwa kuweza kuwa na wazo zuri kama hili la kujenga
kiwanda hapo ndio mnakuwa mnatimiza malengo ya kikosi cha 841kj mafinga
kwa kukuza uzalishaji kwa kutumia raslimali watu ambao mnao katika
kiosi kuzalisha na sio kila siku mnakuwa mnategemea msaada kutoka
serikalini”alisma Chale
Chale
alikitaka kikosi kuendelea kutunza nidhamu waliyonayo na kuendelea
kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuli katika jitihada zake za kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi na
viwanda.
Naye
Bwana shamba wakikosi (farm manager) luteni Francis Breek wa kikosi cha
841kj alisema kuwa wamejipanga kuongeza uzalishaji kwa kuwa wana eneo
kubwa na wana wataalamu wengi wanaoweza kukidhi mahitaji ya kukuza
uzalishaji.
“Ukiangalia
mwaka huu tumelima eneo kubwa na tumeongeza idadi ya mifugo hivyo
tunatarajia kuongeza tena idadi ya mifugo na kupanua eneo la kilimo ili
kuongeza uzalishaji kwa kuwa tumejenga kiwanda na kiwanda kinahitaji
uzalishaji mkubwa wa nafaka pamoja na ufugaji mkubwa na wenye
tija”alisema Breek
Lakini
pia kikosi hicho cha 841kj Mafinga kilizindua jarida linaloitwa uhodari
ambalo linaonesha kila kitu kinachofanywa na kilichofanywa na kikosi
hichotoka kuanzishwa kwake.
“Hongera kikosi cha 841kj kwa Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa kwake”
SHARE
No comments:
Post a Comment