Serikali imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.
Harrison Mwakyembe amesema hayo leo akiwa katika ziara yake mkoani
Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata
takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya
kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.
Pamoja na mambo mengine,
Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na Vifo (RITA),
kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema kuwa bila kuwa
na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa inasababisha nchi
kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.
“Wenzetu nchi zilizoendelea
suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko nyuma, kwa
mfano Mkoa wa Morogoro kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka
2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa
na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa
bado hawasajiliwa,” amesema.
Dk. Mwakyembe pia ametumia
nafasi hiyo kuwaonya watendaji wa mahakama watakaolalamikiwa na wananchi
kufanya kazi kinyume na maadili ikiwamo upokeaji wa rushwa ama
kutotenda haki na kutumia mahakama kugeuza kesi za madai kuwa kesi za
jinai.
SHARE
No comments:
Post a Comment