Korea Kaskazini imewapiga marufuku raia wa Malaysia kuondoka nchini
humo, hatua ambayo Malaysia imesema raia wake wanashikiliwa "mateka"
katika mvutano kuhusiana na kuuawa kwa Kim Jong-Nam. Wizara ya mambo ya
kigeni ya Korea Kaskazini imesema marufuku hiyo itadumishwa hadi pale
usalama wa wanadiplomasia na raia wake nchini Malaysia utakapohakikishwa
kikamilifu kupitia usuluhishi wa haki wa kisa kilichotokea Malaysia.
Hatua hiyo ya kushangaza ya Korea Kaskazini imekuja wakati ambapo
inakabiliwa na shutuma kali kutoka kwa jamii ya kimataifa baada ya
kuvurumisha makombora katika Bahari ya Japan, na kukiuka vikwazo vikali
vya kimataifa vinavyolenga kuusitisha mpango wake wa silaha. Matukio
hayo ya leo yameongeza kabisa mvutano kati ya nchini hizo mbili ikiwa ni
wiki tatu baada ya kaka wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim
Jong-Un kuulkiwa katika uwanja mmoja wa ndege na sumu iliyopigwa
marufuku ya VX ambayo huathiri mishipa ya fahamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment