Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko nchini Somalia
kujadiliana na Rais mpya wa nchi hiyo Mohamed Abdullahi Mohamed kuhusu
baa la njaa linaloikumba nchi hiyo. Guteress amewaambia wanahabri wakati
wa safari yake kuelekea Mogadishu kuwa mzozo, ukame, mabadiliko ya hali
ya hewa, magonjwa na kipindupindu vyote kwa pamoja ni hali ya kutisha.
Katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa atakutana na rais huyo mpya wa
Somalia katika eneo la uwanja wa ndege wa Mogadishu ambalo liko chini ya
ulinzi mkali wa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na ambako
kuna ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutoa misaada ya
kibinadamu. Hiyo ndiyo ziara ya tatu kufanywa na Katibu wa Umoja wa
Mataifa Somalia tangu mwaka 1993, miaka miwili baada ya Rais Siad Barre
kupinduliwa madarakani na kulitumbukiza taifa hilo katika vita vya
wenyewe kwa wenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment