Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewasili mjini Mbabane – Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya
kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC).
Mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini
Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa
na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma
wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo
amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia
vikundi mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA
kwenye mkutano huo.
Hapo
kesho tarehe 17-Marchi-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na
Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC
Double Troika ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika
nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.
Mkutano
huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya
mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika
Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha
ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na
usalama kwenye hizo.
Mkutano
wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo
ambazo ni Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na
Msumbiji.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa
Dakta Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbabane – SWAZILAND.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akikagua gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini
Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa
wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika
(SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiangalia vikundi vya Burudani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa
kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march,16,
2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa
Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais
amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwasili Heshima kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III
mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria
mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa
Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Swaziland alipowasili kwenye
Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo
march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na
serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu
wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
SHARE
No comments:
Post a Comment