Serikali
imewataka viongozi wa kisiasa pamoja na watendaji wa serikali kutotumia
madaraka yao vibaya kuwanyanyasa na kuwasumbua wawekezaji wazawa
waliowekeza ndani ya nchi.
Aidha
viongozi hao wametakiwa kuwaheshimu na kuwajengea mazingira rafiki
yatakayowawezesha kufanya biashara zao kwa amani ili kuweza kukuza
uchumi wa taifa na kuongeza ajira kwa vijana.
Kauli hiyo imetolewa jana
na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda mkoani Simiyu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa
uwekezaji wa mkoa huo pamoja na tovuti ya Mkoa. Prof. Mkenda amewasihi
viongozi wote wa serikali ngazi za mikoa na wilaya nchini kujivunia
uwepo wa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ambao ni wazawa kwani
wao ni chachu ya kuongeza kwa ajira za vijana.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof.
Godius Kahyarara (anayetazama kamera) akibadilishana mawazo na baadhi ya
viongozi wa mkoa wa Simiyu nje ya ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi
wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa
mwongozo wa uwekezaji na tovuti ya mkoa wa Simiyu.(Picha zote na
Thebeauty).
Amesema
kuwa si vyema wafanyabishara kutukanwa, kutolewa lugha zisizokuwa sahihi
na kuonekana kama wana uadui na serikali, na badala yake watukuzwe ili
kuweza kulipa kodi pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi.
“hawa
wafanyabishara hasa wazawa na wajasiriamali tuwaone kama wenzetu, ndugu
zetu na watu muhimu, kwani wameajiri vijana wetu, wanalipa kodi ili nchi
ipate maendeleo, lakini wanatekeleza kauli mbiu ya Rais, Tanzania kuwa
nchi ya viwanda, tuwathamni” alisema Prof.Mkenda. Katibu Mkuu huyo
amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili
ya wawekezaji wakubwa na wadogo kwa ajili ya kujenga viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akisaliana na Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Festo S. Kiswaga mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Kanisa
Katoliki Bariadi, mkoani Simiyu kushiriki uzinduzi wa mwongozo wa
uwekezaji mkoani humo pamoja na kuzindua tovuti ya mkoa huo.
Awali
akizungumza katika sherehe hizo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka
amesema kuwa ili Tanzania iweze kufanikiwa katika azma yake ya kuwa na
viwanda lazima serikali iwekeze kwanza katika utafiti wa fursa
zilizopo.
Amesema
kuwekeza katika utafiti utasaidia kutoa uthubutu wa kufanya na kutenda
mambo mbalimbali yatakayoifanya nchi kuwa na uchumi wa kati na kuwaletea
wananchi maendeleo. “nchi hii tusingelihitaji kuona wakuu wa mikoa kuwa
wabobezi katika kila sekta na badala yake wawaache wataalam na watafiti
wafanye kazi zao kitaalamu ili kuepuka mvurugano wa shughuli za
kimaendeleo ndani ya nchi” amesema Mtaka.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akitoa utambulisho wa
meza kuu na maelezo ya lengo la mwongozo wa uwekezaji katika sherehe
hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani
Simiyu.
Kwa
upande wake Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian
Bamwenda, amesema kukamilika kwa utafiti huo mkoani Simiyu utatoa fursa
kwa wananchi na wafanyabishara kutambua wapi kuna fursa sahihi na haraka
kuwekeza.
Utafiti
huo ulifanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) kati ya
mwezi Januari na Februari mwaka huu mkoani humo kwa ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambapo zaidi ya shilingi Milioni
60 zilitumika katika utafiti huo na kubaini uwepo wa fursa 26.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni
rasmi na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji
mkoani humo ulioratibiwa na ESRF chini ya ufadhili wa UNDP.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye sherehe ya uzinduzi wa
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu ulioenda sambamba na uzinduzi wa
tovuti ya mkoa wa Simiyu.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian
Bamwenda akitoa wasilisho la fursa za uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa
sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian
Bamwenda akiitambulisha timu iliyoshiriki kwenye utafiti huo. Kutoka
kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi
(ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF,
Bi. Margareth Nzuki, Afisa wa Habari Mwandamizi wa ESRF, Abdallah Hassan
pamoja na UNDP Programme Specialist, Amon Manyama.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP)
nchini ambao ndio wafadhili wa utafiti huo, Awa Dabo akitoa salamu za
UNDP wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani
Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF),
Dkt. Tausi Kida akitoa salamu za ESRF wakati wa sherehe za uzinduzi wa
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa
Katoliki Bariadi.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Antony Mtaka wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji
mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof.
Godius Kahyarara akitoa salamu za NSSF wakati wa sherehe za uzinduzi wa
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu uliofanyika katika Kanisa Katoliki
Bariadi.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda akisaidiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka kukata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu
uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani Simiyu.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka wakionyesha
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu baada ya kuzindua.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu kwa ajili ya utekelezaji wakati wa
hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo ulioratibiwa na ESRF chini ya ufadhili
wa UNDP.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda (katikati) akimkabidhi nakala Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini Awa Dabo ambao ndio
wafadhili wa utafiti wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoani Simiyu.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda (wa pili kushoto) akikabidhi nakala ya mwongozo wa
uwekezaji mkoani Simiyu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda (wapili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara nakala ya
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa
mwongozo huo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi,
Mkoani Simiyu.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda akiabidhi nakala hizo kwa watendaji wa mkoa wa Simiyu.
Kikundi cha Kwaya ya Simiyu kikiimba wimbo maalum wa kuhamasisha
uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa
uwekezaji mkoani Simiyu.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP) nchini ambao ndio wafadhili wa utafiti huo, Awa Dabo,
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini, Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda wakitazama burudani
ya kwaya kutoka mkoani Simiyu kwenye sherehe za uzinduzi huo. Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu katika sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya viongozi wa mkoa wa Simiyu,
Wafanyabiashara, Wanahabari, Viongozi wa madhehebu ya dini pamoja
wawekezaji waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji
wa mkoa wa Simiyu. Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu. Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ESRF na UNDP. Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji wa mkoa wa Simiyu. Meza kuu katika picha ya pamoja na madiwani wa mkoa wa Simiyu. Meza kuu katika picha ya pamoja na kwaya ya mkoa wa Simiyu. Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Simiyu. Meza kuu katika picha ya pamoja na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP)
nchini,, Awa Dabo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara
baada ya kumalizika sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani
Simiyu.
No comments:
Post a Comment