
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya
Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 Mwaka huu, katika
uwanja wa Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana maadhimisho
hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali, na
yataanzia katika Shule ya Msingi Mabatini kuelekea viwanja vya
Mwembeyanga.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.
Kauli mbiu hiyo inalenga
kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa
Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya
jamii kwa ujumla.
Taarifa hiyo pia imeikumbusha
jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na
kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili
wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda.
Maadhimisho hayo yataambatana na
maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa
Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya wanawake
vitaonesha bidhaa zao.
Aidha, Wananchi wa Mkoa wa Dar es
salaam wanakumbushwa kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo
ikiwa ni pamoja na kuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto
mbalimbali zinanazowakabili Wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.
SHARE
No comments:
Post a Comment