Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi
pamoja na Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya Wizara yake mkoani humo.
Katika mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
kuanzisha Kituo cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi Aprili mwaka
huu pamoja maandilizi ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauniakimpa maelekezo
Fundi Mkuu wa ujenzi wa Gereza Ruangwa (kushoto) wakati Naibu Waziri
huyo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo unaoendelea mjini Ruangwa.
Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Tusekile Mwaisabila.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia)
akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ruangwa, Joseph Kiyengi
wakati alipokuwa akionyesha eneo litakalojengwa Kituo kipya cha Polisi
wilayani humo. Maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho yameshaanza. Katika
ziara yake Masauni pia aliagiza uanzishwaji wa Kituo cha Zimamoto
wilayani humo haraka iwezekanavyo. Katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya
hiyo, Twaha Mpembenwe.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya
Ruangwa, Joseph Kiyengialipokuwa anatoa taarifa yake katika Kikao cha
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa ambacho
kilijumuisha Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya Wizara hiyo mkoani Lindi.
Katika mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
kuanzisha Kituo cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi Aprili mwaka
huu pamoja maandilizi ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment