Mawaziri wa fedha wa nchi zenye nguvu za kiuchumi na zinazoinukia
kiviwanda G20 wanakutana Ujerumani hii leo huku kukiwa na wasiwasi
kuhusu kuongezeka kwa malumbano ya kibiashara kutokana sera ya Rais wa
Marekani Donald Trump ya kutanguliza maslahi ya Marekani.Hapo jana,
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa China Xi Jinping walitoa
tamko la pamoja wakiahidi kuwa kwa pamoja watapigania biashara huru na
masoko ya wazi. Waziri mkuu wa China Li Keqiang pia ameionya Marekani
akisema hawataki vita vya biashara kati ya nchi hizo mbili.Ujerumani
ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo wa mawaziri wa fedha inatafuta kuondoa
suala la biashara kutoka taarifa ya mwisho itakayotolewa mwishoni mwa
mkutano huo wa siku mbili hadi pale viongozi wa nchi watakapokutana kwa
mkutano wa kilele wa G20 mwezi Julai. Mkuu wa shirika la fedha duniani
IMF Christine Lagarde amezihimza nchi za G20 kujiepusha na kujidhuru
wenyewe kwa kujitenga na sera zitakazoathiri biashara, uhamiaji na
kubadilishana teknolojia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment