Polisi mjini Brussels wamemkamata mwanamke mmoja anayetuhumiwa
kuwasaidia watu wanaopanga kufanya mashambulizi mahala fulani barani
Ulaya. Waendesha mashtaka wamesema leo kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa
miaka 24 aliyefahamika kwa jina la Molly B alikamatwa katika msako wa
polisi uliofanyika usiku kucha mnamo Machi 7. Molly anakabiliwa na
mashtaka ya kushirikiana na kundi linaloendeleza vitendo vya kigaidi.
Hata hivyo kesi hiyo haifungamanishwi na shambulio la mwaka 2015 la
mjini Paris, Ufaransa au mashambulio ya kujitoa muhanga yaliyofanywa
katika uwanja wa ndege na katika kituo cha treni mjini Brussels. Vyombo
vya usalama nchini Ubelgiji vimeweka ulinzi mkali tangu mashambulio hayo
yalipotokea ambapo watu 32 waliuwawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment