Ujerumani na Urusi zimefikia makubalino kwamba Shirika la Ushirikiano
na usalama barani Ulaya OSCE lazima liwe na uwakilishi madhubuti katika
maeneo ya mizozo huko mashariki mwa Ukraine. Waziri wa mambo ya nje wa
Urusi Sergei Lavrov na mwenziwe wa Ujerumani Sigmar Gabriel waliyasema
hayo kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya kumaliza
mkutano wao mjini Moscow. Hata hivyo viongozi hao wameelezea kwamba zipo
tofauti baina nchi zao kuhusu mitazamo yao kwenye mgogoro huo ambapo
wapiganaji waliotangaza kujitenga na wanaoipendelea Urusi wanapambana na
majeshi ya Ukraine kwa muda wa miaka mitatu sasa. Waziri Sigmar Gabriel
amezilaumu pande zote mbili kwa kukiuka makubaliano ya kuziondoa silaha
nzito na pia ameilaumu Urusi katika hatua yake ya kuzikubali stakabadhi
za kusafiria pamoja na vielelezo vingine vya wanachama wa kundi
lililotangaza kujitenga. Lavrov kwa upande wake ameilaumu serikali ya
Ukraine kwa kuendeleza mapigano.
Thursday, March 9, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment