Na Eleuteri Mangi, MAELEZO
Baraza
la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi
kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa
kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.
Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti ambavyo sio vyao.
Kwa
mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au
taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine
kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.
Wananchi
wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa
saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu
hadi Ijumaa.
Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia barua pepe helpdesk@necta.go.tz au simu namba 0658 116 644 kwa saa za kazi.
Tangazo
hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu
wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa
watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake.
SHARE
No comments:
Post a Comment