Wapalestina na Umoja wa Mataifa leo wamelaani hatua ya baraza la
mawaziri la Israel kuidhinisha ujenzi wa makaazi ya walowezi katika eneo
wanalolikalia la Ukingo wa Magahribi kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya
miaka 20.
Jana baraza la mawaziri wa usalama limeunga mkono kwa kauli
moja ujenzi huo mpya, ambao unaonekana kama serikali ya mrengo wa kulia
katika historia ya Israel inashikiza kuendelea na upanuzi wa makaazi
bila ya kujali wito wa kimataifa.
Afisa mwandamizi wa Palestina, Hanan
Ashrawi amesema hatua hiyo inayoonyesha kuwa serikali inaendeleza sera
zake kuhusu ukoloni wa walowezi, ubaguzi wa rangi na mauaji ya safisha
safisha, inaonyesha wazi jinsi isivyoheshimu haki za watu wa Palestina.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gueterres, ameelezea
kusikitishwa kwake na tangazo hilo.
No comments:
Post a Comment