Raia tisa wa Malaysia waliokuwa wanashikiliwa Korea Kaskazini
wamerejea nyumbani mapema leo asubuhi, baada ya serikali kuutoa mwili wa
Kim Jong Nam, kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
Kubadilishana huko kumemaliza mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya nchi
hizo mbili kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya Kim kuuawa katika uwanja wa
ndege wa Kuala Lumpur.
Kufuatia mazungumzo ambayo yameelezwa kama
''muhimu sana'', Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak amekubali kuuachia
mwili huo kwa masharti ya kurejea nyumbani raia tisa wa Malaysia
waliokuwa wanashikiliwa Pyongyang.
Mauaji ya Kim yaliyofanyika Februari
13 kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur yamezusha uvumo kwamba huenda
Korea Kaskazini ilituma kikosi chake kwa ajili ya kutekeleza mauaji
hayo.
SHARE
No comments:
Post a Comment