Kiongozi wa Umoja wa Ulaya atakayesimamia zoezi la kumchagua rais
mpya wa Baraza la Ulaya amesema rais wa sasa Donald Tusk ana nafasi
nzuri ya kuchaguliwa tena kwa sababu anaungwa mkono kwa kiwango kikubwa.
Waziri mkuu wa Malta Joseph Muscat amesema saa chache kabla ya mkutano
wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuanza kwamba hata kama kuna
nchi ambazo haziridhishwi kutokana na kushikiliwa nafasi zote za muhimu
na wanachama wa kundi la Christian Democrats katika Umoja wa Ulaya na
hiyo haitakuwa sababu ya wao kumpoteza rais wa sasa wa kamisheni hiyo
Donald Tusk kwa sababu wao wanauhakika kuwa amefanya kazi nzuri. Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuchaguliwa tena kwa Donald Tusk ni
ishara ya utulivu katika Umoja wa Ulaya. Wakati huo huo waziri mkuu wa
Poland amesema nchi yake itafanya kila jitihada kuzuia kuchaguliwa tena
Donald Tusk. Poland badala yake inampendekeza Jacek Saryusz-Wolski
(YACHEK SARYUJ-VOLSKI) ambaye hajulikani._
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment