MAJIMBO ya Ujerumani yamewaonya Waturuki wanaoishi humu nchini kwamba
Uturuki inawachunguza au kuwapiga picha kwa siri.
Hayo ni kwa mujibu wa
gazeti la Ujerumani la Süddeutsche Zeitung.
Idara ya Ujasusi ya Uturuki
MIT imekusanya orodha na taarifa kuhusu mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa
wafuasi wa imamu wa kiislamu Fethullah Gülen wanaoishi Ujerumani na
kuziwasilisha kwa serikali mjini Berlin.
Gazeti hilo limesema orodha hiyo
inajumuisha majina, anwani, nambari za simu na picha zilizopigwa
kutumia kamera za siri.
Orodha hiyo inawatambua watu zaidi ya 300 na
vilabu 200, shule na taasisi nyingine zinazoshukiwa kuwa na mafungamano
na Güllen anayeishi uhamishoni nchini Marekani.
Ujerumani inaichunguza
orodha hiyo kujua jinsi idara ya ujajusi ya Uturuki ilivyopata taarifa
hizo.
No comments:
Post a Comment