TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania za kupiga marufuku unywaji na uuzwaji wa pombe hasa zile zilizofungwa
kwenye mifuko aina ya viroba ziambatane na uundwaji wa sera ya pombe ya Taifa itakayosaidia katika kudhibiti
matumizi ya vilevi hapa nchini.
Sera ya hiyo italazimisha sheria zinazoambatana kurekebishwa ambapo pia zitawawezesha wafanyabiashara,
watengenezaji na wauzaji wa kinywaji hicho kutambua haki, madhara na makosa yao
mapema katika utoaji huduma, na hiyo itaisaidia serikali katika usimamizi
madhubuti, na mwenendo wa udhibiti utakuwa wazi tofauti na sasa ambapo serikali imeamua kupiga marufuku kwa
kushtukiza, jambo ambalo limepelekea kuleta
madhara kwa wafanyabiashara ambao kwa namna moja au nyingine hawakuwa wanajua
madhara yake.
Matumizi ya pombe aina ya viroba hayana budi kuwekewa
sera, na sheria ziboreshwe hasa juu ya matumizi kwani yanachangia madhara makubwa
ya kiafya kwa jamii pamoja na ukatili wa
kijinsia kwa wanawake na watoto, migogoro majumbani, utelekezaji wa familia,
ubakaji, ajali barabarani na pengine kuharibu nguvu kazi ya jamii na taifa kwa
ujumla
Chama cha Wanahabari Wanawake – TAMWA, kupitia kupitia
kituo chake cha usuluhishi (CRC), kimekuwa kikiomba uwepo wa sera ya Taifa juu
ya matumizi ya Pombe nchini kama ilivyo nchini Kenya na Uganda, aidha kimekuwa
kikitoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya pombe kupita kiasi ambapo kwa mwaka
2016 kiliweza kuwapa ushauri nasihi wananchi wapatao 490, kati ya hao wanawake
walikuwa 355, wanaume 92 na watoto walikuwa 45 walioathirika kwa namna
mbalimbali kutokana na unywaji pombe kupindukia.
Edda Sanga
Mkurugenzi Mtendaji
SHARE
No comments:
Post a Comment