NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, ameipongeza kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC kuwa ya kwanza kutekeleza sheria
ya EPOCA na sheria ya fedha ya mwaka 2016 kwa kuuza hisa zake kwa Umma
kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na alitoa rai kwa
watanzania,makampuni ya kitanzania na taasisi za serikali kujitokeza
kununua hisa hizo baada ya kusoma waraka wa matarajio
wenye mwongozo wa ununuaji wa hisa za kampuni hiyo.
Akiongea
wakati wa Uzinduzi wa uuzaji wa hisa za kampuni hiyo uliofanyika
jijini Dar e salaam, Dk. Kijaji alisema kuwa uwekezaji huu utakuza
shughuli za soko kwa asilimia kubwa “Hivi sasa wawekezaji katika hisa
kwenye masoko ya mitaji hapa nchini ni takribani laki tano,hivyo iwapo
wateja wote wa Vodacom milioni 12.4 watashiriki katika ununuzi wa hisa
utaongeza uwekezaji wa hisa kupitia masoko ya
mitaji katika soko la hisa kwa asilimia 2,380%.
Alisema
haya yatakuwa ni mageuzi makubwa katika sekta ya masoko ya mitaji na
fedha si hapa nchini tu bali hata katika ukanda wa Afrika Mashariki
kwani hivi sasa Kenya ina wawekezaji wapatao 1,700,000,Uganda 40,000 na
Rwanda 14,000.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao
amesema, “Tunayo furaha kuifikia siku ya leo ambapo tumefungua milango
kwa wananchi wa Tanzania na tunawakaribisha wanaotaka kuwekeza katika
safari hii ambayo tumeianza.Tukio hili ni la kihistoria katika sekta ya
mawasiliano nchini Tanzania, Vodacom Tanzania imekuwa kampuni ya kwanza
ya mawasiliano hapa nchini kuandika historia
ya kuuza hisa zake kwa umma kupitia Soko la benki ya NBC yenye matawi
nchi nzima na mawakala kwa kuuza hisa kuwashirikisha watanzania wote
katika safari ya mafanikio ya kampuni yetu”.
Ferrao
alisema kuwa kuanzia leo,asilimia 25% za kampuni ya Vodacom Tanzania
PLC zitauzwa kwa watanzania kutokana na kibali kutoka serikalini
kupitia Mamlaka ya Dhamana Masoko na mitaji (CMSA)-“Kutokana na matakwa
ya sheria hadi kufikia hatua hii tumepata ushirikiano mkubwa kutoka
taasisi za serikali za CMSA ,DSE na wadau wengine,nashukuru kwa
ushirikiano huu ambao umefanikisha mchakato mzima na
leo wateja wetu nchini kote na taasisi mbalimbali za kitanzania zinazo
fursa ya wabia wetu kupitia ununuaji huu wa hisa”Aliongeza.
Kuhusiana
na mchakato mzima wa ununuaji wa hisa alisema “Kutokana na kuzinduliwa
mchakato wa uuzaji hisa kuanzia leo,wanaohitaji kununua hisa
watazipata kwa kutembelea matawi yote ya Benki ya NBC na mawakala wa
Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) waliopo nchi nzima “.Alitoa
msisitizo kuwa kila hisa itauzwa kwa shilingi 850/-na asilimia 25% ya
hisa zinazotarajiwa kuuzwa zina thamani ya shilingi
Bilioni 476.
Ferrao
alimalizia kwa kusema “Vodacom Tanzania PLC inayo dhamira ya kweli ya
kuendelea kuwekeza nchini na kukuza sekta ya mawasiliano na kufanikisha
malengo yake makuu ambayo ni kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa
kidigitali,kuwaunganisha watanzania katika mtandao wake na kubadilisha
maisha ya wananchi kuwa murua kupitia ubunifu mkubwa wa kiteknolojia.
SHARE
No comments:
Post a Comment