TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama
cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika yanayotetea haki
za binadamu hasa wanawake na watoto ulimwenguni kusherekea siku ya wanawake
duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka.
Kauli
mbiu kitaifa mwaka huu ni “Tanzania ya Viwanda: Mwanamke ni Msingi wa
Mabadiliko Kiuchumi” ambayo inatutaka wote tushiriki kikamilifu katika
kuleta mabadiliko ya mitazamo, fikra na matarajio ya kimaendeleo hasa kwa wanawake.
Aidha kauli mbiu ya mwaka huu inatazamia serikali na wanasheria kuboresha sera
na sheria ili ziweze kuleta uwezo wa ustawi na kuwawezesha wanawake wawe na uwezo
wa kufikia mabadiliko yao ndani ya familia
na kuleta usawa katika maamuzi .
Inakadriwa
kuwa duniani kote ni asilimia 50 tu ya wanawake ambao wanajishugulisha na kazi
rasmi ikilinganishwa na asilimia 76 ya wanaume. Aidha kazi nyingi ambazo
zimekuwa zikifanywa na wanawake ni za hali ya chini na zinawaingizia kipato
duni.
TAMWA
inaamini kuwa azma ya nchi ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati na
viwanda itafikiwa endapo haki ya elimu
kwa mtoto wa kike itapewa kipaumbele na kuhakikisha sera na sheria kandamizi
kwa wanawamke na watoto wa kike zitarekebishwa na kuwezesha ushirikishwaji wa
wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi na maamuzi.
Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani yana lengo la kuwezesha jamii kupima utekelezaji wa
maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa/ kikanda
na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika
kuhakikisha haki za wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa zinapatikana na
zinalidwa.
Edda
Sanga
Mkurugenzi
Mtendaji
SHARE
No comments:
Post a Comment