Vodacom yawapiga msasa mawakala watakaokusanya fedha za hisa
Mawakala
wa kuuza hisa za Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, wamepatiwa mafunzo elekezi ya
siku moja iliyokuwa na lengo la kuwaelimisha mawakala hao jinsi ya
kukusanya fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa za kampuni hiyo
litakapoanza hivi karibuni kwani limekuwa likisubiriwa kwa
hamu kubwa na watanzania walio wengi.
Semina
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City
ambapo uongozi wa kampuni ya Vodacom Tanzania na mawakala walipata fursa
ya kubadilishana mawazo kuhusiana na mchakato mzima wa zoezi hilo
utakavyoendeshwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo, Ian Ferrao alisema “Tunawashukuru kwa
ushirikiano wenu tangia tulipoanza mchakato wa maombi ya kuuza hisa
kwa umma hadi kufkia sasa ambapo tayari tumepata kibali cha kutekeleza
zoezi hili kutoka serikali kupitia Mamlaka ya Dhamana Masoko na mitaji
(CMSA) na mkiwa wabia wetu katika mchakato huu tumewaita kwa ajili ya
kubadilishana mawazo jinsi tutakavyofanikisha
matarajio yetu tuliyokusudia na kuwa tayari kwa kazi iliyosubiliwa kwa
muda mrefu”.
Ferrao
alieleza kuwa Vodacom inatarajia kuuza asilimia 25% ya hisa zake kwa
umma zenye thamani ya shilingi Bilioni 476/-na kila hisa itauzwa
kwa shilingi 850/-
Vodacom
Tanzania PLC,imekuwa ya kwanza kutekeleza sheria ya Electroniki na
Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya fedha ya mwaka 2016
inayoyataka
makampuni kumilikisha asilimia 25% ya hisa zake kwa umma kupitia Soko
la Hisa la Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Ferrao, wananchi wataweza kununua hisa za zao katika matawi
ya Benki ya NBC na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)
waliopo
nchini kote.
Wakati
zoezi la uuzaji hisa za Vodacom linatarajiwa kuanza rasmi hivi
karibuni,wawekezaji na wananchi wamekuwa wakisubiri kwa shauku kubwa
ambapo
wamekuwa wakifuatilia kwa karibu jinsi zoezi hili linavyoendelea ili
waweze kujipatia fursa ya kumiliki hisa katika kampuni kinara ya
mawasiliano nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment