Julian Msacky
“KAMA ulimwengu ukiwachukia ninyi kumbukeni umenichukia mimi
kabla ya yenu”.
Haya ni maneno ya Yesu katika moja ya mahubiri yake ambapo
alihimiza wanafunzi wake kuishi kwa upendo.
Aliwakumbusha kuwapenda hata wale ambao hawawapendi kwani
hakuja kwa ajili ya watu wema bali wenye dhambi.
Katika mahubiri yake alisisitiza watu kuishi kwa upendo, kuacha
chuki, uhasama na visasi visivyo na msingi.
Rais John Magufuli akisisitiza umuhimu wa kutunza amani ya nchi
Ni kwa nini? Ni kwa sababu penye chuki hakuna upendo. Penye visasi amani hutoweka na umoja huyoyoma.
Ni kwa nini? Ni kwa sababu penye chuki hakuna upendo. Penye visasi amani hutoweka na umoja huyoyoma.
Penye uhasama uadui hutawala. Inapofikia hapo watu huishi kwa
hofu kwa maana ya Ibilisi kusimika mizizi.
Alikwenda mbali zaidi na kuhoji kama “mkiwapenda wale
wanaowapenda tu mwapata thawabu gani?”
Hii ni kuonesha ni aina gani ya maisha ambayo wanadamu wanatakiwa
kuishi bila kujali ana madaraka au la.
Ndicho tunachofundishwa leo hii hasa ikizingatiwa wenye
mamlaka na wasio nayo wanatakiwa kuheshimiana.
Kwa kufanya hivyo umoja, upendo na mshikamano ndani ya jamii utatawala
na amani ya kweli kushamiri zaidi.
Hayati Mwalimu Julius Nyerere alitupitisha katika mambo hayo
na kusema kweli nchi ilisimama.
Nchi ilijipatia heshima na wananchi vivyo hivyo.
Hatukuparuana sisi wenyewe au kuoneshana umwamba.
Palipotokea tofauti zilitatuliwa kwa njia za amani na mambo
yakaendelea kama kawaida. Hii ndiyo zawadi aliyotuachia.
Mwalimu alijenga taifa lenye mshikamano, umoja na amani.
Hakuruhusu kupanda mbegu ya chuki.
Ni kwa sababu hiyo amekuwa kiongozi wa kipekee wa kisiasa kuingia
kwenye mchakato wa kuitwa mtakatifu.
Pamoja na madaraka yake Nyerere alijishusha. Hakujikweza.
Alikemea viongozi waliotumia madaraka vibaya.
Kama si umakini wa Mwalimu Nyerere na kuhimili siasa za
ushindani, leo hii tusingekuwa na vyama vingi vya siasa.
Nyerere alikuwa na ngozi ngumu. Alihimili majaribu. Alikemea
viongozi kuacha kuacha kuumbuana wenyewe.
Alitambua kufanya hivyo ni kukaribisha uadui na kuteteresha
umoja na mshikamano kati yao na nchi.
Waliokosea waliwajibishwa kwa taratibu zinazotakiwa na hakuwa
na mchezo na wala rushwa.
Ni kwa sababu hiyo jina lake linaendelea kukumbukwa kuanzia na
watoto wadogo hadi wakubwa.
Kwa lugha nyingine Nyerere alikuwa kimbilio kwa waliokata
tamaa na pia hakujenga nyufa ndani ya nchi.
Hakuishia hapo. Alikemea tabia ya baadhi ya viongozi kutaka
kujikweza, kuabudiwa na kujiona miungu watu.
Viongozi wetu wana mengi ya kujifunza kutoka kwa Nyerere. Kwa
kufanya hivyo tutasafiri salama.
Tutahimili mawimbi hata yanapotokea na kutishia umoja wetu
kama taifa.
Tunaamini kwa kuunganisha nguvu zetu na kumtanguliza Mungu
mbele tutaepuka chuki na kuhubiri upendo.
Nimetumia maneno ya Yesu na nasaha za Nyerere ili kuonesha
namna gani tunatakiwa kuishi ndani ya nchi yetu.
Hii ikiwa na maana kwa namna tunavyofanya mambo yetu, lakini
pia namna tunavyoshughulikia matatizo.
Kimsingi ni lazima tuhakikishe kila tunachofanya hakileti
mpasuko ndani ya jamii kwani kuna leo na kesho.
Ndiyo kusema viongozi wetu wana jukumu la kutuongoza kwa
misingi iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.
Tunachojivunia miaka yote si utajiri uliopo nchini. Si ukubwa
wa nchi au idadi ya watu waliopo, la hasha.
Jambo ambalo tunajivunia ni amani, upendo na mshikamano. Hizi
ndizo tunu muhimu ndani ya nchi yetu.
Tunu hizi zikitoweka hata tuwe na mali kwa kiwango gani ni
kazi bure. Hata tupige vita rushwa vipi ni kazi bure.
Bila tunu hizo mfumo wetu wa siasa utakuwa ni kazi bure.
Ndiyo maana nasisitiza tuzilinde.
Wanasiasa na mihemko yao ya kisiasa watapita, lakini nchi
itaendelea kuwepo hivyo lazima tupiganie amani yetu.
Tupendane sisi kwa sisi. Wanasiasa wapendane. Wasiishi kwa
chuki na visasi. Wasioneane wao kwa wao.
Wanatakiwa wawe mfano mzuri kwa wananchi wakifahamu siasa si
mbaya bali ni mbaya kwa wasiasa wabaya.
Hivyo viongozi watimize majukumu yao vizuri kwa wananchi.
Kamwe wasitumie nafasi au vyeo vyao vibaya.
Wenye masikio na wasikie. Siku zitakuja ambapo kila mmoja
ataulizwa namna gani alivyotumia nafasi yake.
Mtakaposikia habari hizo msitaharuki kwa sababu siku ya
mwisho kutakuwa ni “kilio na kusaga meno”.
Hii ni changamoto kwa kila mmoja wetu kuhakikisha anatumia
kipaji au cheo chake kwa ustawi wa jamii pana na si kuleta uadui au
mfakarakano.
SHARE
No comments:
Post a Comment