Kiasi ya watu 48 wameuawa katika maporomoko ya taka yaliyotokea
katika jalala kubwa kwenye viunga vya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Msemaji wa jiji la Addis Ababa, Amare Mekonen amesema leo kuwa watoto
15 ni miongoni mwa waliouawa. Mamia ya watu wanaishi katika eneo hilo la
jalala la Reppi ambalo liko kwa miaka 50 sasa. Hilo ni eneo pekee la
kutupa taka katika mji huo, ambako pia watu huokota chakula na eneo
ambalo pia vinapatikana vitu vinavyoweza kutumiwa kwa matumizi mbadala.
Watu 28 wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu hospitali. Mekonen
amesema katika juhudi za kuzuia tukio kama hilo kutokea tena, watu
wanaoishi kwenye eneo hilo, wamepelekwa katika vituo vya vijana katika
maeneo mengine ya mji huo mkuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment