Wataalam zaidi ya 130 wa siasa ya nje wa Marekani wanapinga amri mpya
ya rais Donald Trump inayowazuwia watu kutoka mataifa sita ya kiislam
kuingia nchini humo. Wataalam hao wanaitaja amri hiyo kuwa ni ya "hatari
kwa usalama wa taifa." Katika waraka walioitumia serikali mjini
Washington, wataalam hao wanahoji kwamba uamuzi wa rais Trump kuwapiga
marufuku waislam kuingia Marekani, unaikuza propaganda isiyokuwa na
msingi kwamba Marekani inapigana "vita dhidi ya dini ya kiislam".
Miongoni mwa waasisi wa waraka huo ni pamoja na waziri wa zamani wa
mambo ya nchi za nje wa Marekani Madeleine Albright, mshauri wa zamani
wa masuala ya usalama wa taifa Susan Rice, waziri wa zamani wa usalama
wa taifa Janet Napolitano na kiongozi wa zamani wa kituo cha kinga dhidi
ya ugaidi Matthew Olsen. Balozi wa zamani wa Marekani katika jumuia ya
kujihami ya NATO Nicholas Burns na msimamizi wa zamani wa rais wa zamani
George W. Bush katika mapambano dhidi ya ugaidi Richard Clarke ni
miongoni pia mwa waliotia saini waraka huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment