Siku
chache baada ya staa mwimbaji Diamond Platnumz kuzindua Perfume yake
mpya “Chibu Perfume” na kuonesha kupokelewa kwa nguvu kubwa nchini
Tanzania, Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangalla ameandika ujumbe
kuhusu perfume hiyo huku akimsifia Diamond kwa kufanya vitu vikubwa
pamoja na kukiri kuwa yeye sio shabiki wake isipokuwa anaupenda muziki
wake.
“Sikuwahi
kuwa mshabiki wa msanii huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema
hapo nyuma kidogo, japokuwa nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki
wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia nimegundua kuwa, this young man is
not only a good entertainer, but also a talented entrepreneur and
businessman.
He
does business in music, he does a business of entertainment. Sasa naona
kupitia kipaji chake cha ujasiriamali, naona ameamua kuwa muwekezaji,
an investor! This is incredible. Keep stepping up your game son, that’s
the way to do it! Hakika wewe umetoka #NjeYaBox, na Mungu akuongoze
ubaki huko huko juu, usishuke!
I
wish wasanii wenzako pia watoke nje ya box kifikra, wafanye biashara
kwenye vipaji vyao, wageuze changamoto kuwa fursa, waache kulalamika,
wapige kazi tu! #HapaKaziTu! Kwa sababu nyie watu mashuhuri mkigeuza
crowds zenu kama chanzo cha solo la bidhaa zenu, kwa hakika mtafanikiwa
sana!
Changamoto kwenu wadogo zangu…#chibudangote #chibu #diamondplatnumz
SHARE
No comments:
Post a Comment