DESEMBA
2017 inatarajiwa kuwa siku ya kihistoria kwenye sekta ya afya na tiba
duniani ambapo utafanyika upasuaji wa kupandikiza kichwa kwa mara ya
kwanza utakaofanyika mjini London ikihusisha madaktari 150 na itachukua zaidi ya saa 34.
Kwa mujibu wa Daktari atakayeongoza upasuaji huo Dr. Sergio Canavero, upasuaji
huo utafanyika kwa mara ya kwanza kwa binadamu ambapo kichwa cha
binadamu aliye hai kitapandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa na
binadamu huyo kuweza kupata mwili mpya.
Madhumuni ya upasuaji huu ni kusaidia watu waliopata magonjwa ya kupooza
viungo, watu wenye vilema vya miguu na magonjwa ya uti wa mgongo kupata
matumaini mapya ya kuwekewa mwili mwingine. Upasuaji huu unatajwa
kugharimu zaidi ya Dollar millioni 30.
Upasuaji utafanywa kwa mara ya kwanza kwa mgonjwa Valery Spiridonov kutoka Urusi ambaye
kitaondolewa kichwa chake na kupandikizwa kwenye mwili wa mtu
aliyekufa. Valery Spiridonov amejitolea kufanyiwa upasuaji huou kwa
sababu ana tatizo la uti wa mgongo liliopelekea mwili wake kupata
ugonjwa wa kiharusi.
VIDEO:Ulipitwa na huu utafiti kuhusu dawa ya uzazi wa mpango ya panya kutumika kwa binadamu?Bonyeza play kutazama
SHARE
No comments:
Post a Comment