Wakati Korea Kaskazini ikiendelea kufanya majaribio ya makombora ya
masafa ya kati, chama tawala nchini Japan cha waziri mkuu Shinzo Abe
kinatafakari kujenga uwezo wa kushambulia vituo vya adui.
Korea
Kaskazini hivi karibuni imeimarisha progamu zake za nyuklia na
makombora, ambapo katika mwaka uliopita pekee ilifanya majaribio mawili
ya nyuklia na mengine 20 ya makombora ya masafa marefu.
Mapema mwezi
Machi Pyongyang alifanya majaribio ya makombora manne, ambapo matatu
kati yake yaliangukia katika eneo la bahari linalomilikiwa na Japan.
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Japan Itsunori Onodera anaanimini Korea
Kaskazini makombora yenye uwezo mkubwa.
Waziri mwingine wa zamani wa
ulinzi Jenerali Nakatani, alikaribisha hatua ya Marekani kuweka mfumo wa
ulinzi dhidi ya makombora nchini Korea Kusini na kuongeza kuwa ni
muhimu kusihirikiana na mataifa hayo mawili ili kushghulikia kitisho
kinachoongezeka cha Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment