Rais
mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, (katikati), akiwa na Katibuwa
Bunge Dkt. Thomas Kashilila, (kushoto), na Katibu Mnyeka wa Spika wa Bunge,
Bw.Said O. Yakubu, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo Aprili 4, 2017.
Dkt. Kikwete akiwa na familia yake, alifika bungeni hapo kumsindikiza mkewe
Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa anakula kiapo cha kuwa mbunge baada ya
kuteuliwa na Rais, Dkt. John Magufuli.
NA K-VIS BLOG, DODOMA
RAIS
Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo Aprili 4, 2017
amelifanya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoanza vikao vyake mjini Dodoma "kutikisika" baada ya nderemo, vifijo kulipuka baada ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, aliposimama kumtambulisha kwa wabunge.
Kupitia matangazo ya moja kwa moja ya
runinga kutoka Bungeni mjini Dodoma, Mhe. Ndugai alisema "tuna mgeni
maalum hapa Bungeni nae si mwingine ni
Rais mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete"
Baada ya utambulisho huo ndipo vifijo vilipolipuka toka kwa wabunge wote wa CCM na upinzani ambapo wengine walisikika wakisema “tumeku-miss sana na tunakukumbuka.”
Dkt. Kikwete akiwa na baadhi ya watoto wake, alimsindikiza mama Salma
ambaye ameapishwa leo kuwa mbunge kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kumteua kuwa mbunge hivi
karibuni.
SHARE
No comments:
Post a Comment